-
Roho ya Yehova Huwaongoza Watu WakeMnara wa Mlinzi—1992 | Septemba 15
-
-
Jinsi Ambavyo Roho Husaidia
9. (a) Roho takatifu hutumikaje ikiwa “msaidizi”? (b) Tunajuaje kwamba roho takatifu si mtu? (Ona kielezi-chini.)
9 Yesu Kristo aliiita roho takatifu “msaidizi.” Kwa mfano, aliwaambia wafuasi wake hivi: “Nitamwomba Baba, naye atawapa Msaidizi mwingine, ili akae nanyi hata milele; ndiye Roho wa kweli; ambaye ulimwengu hauwezi kumpokea, kwa kuwa haumwoni wala haumtambui; bali ninyi mnamtambua, maana anakaa kwenu, naye atakuwa ndani yenu.” Miongoni mwa mambo mengine, “msaidizi” huyo angekuwa mwalimu, kwani Kristo aliahidi hivi: “Msaidizi, huyo Roho Mtakatifu [roho takatifu, NW], ambaye Baba atampeleka kwa jina langu, atawafundisha yote, na kuwakumbusha yote niliyowaambia.” Roho hiyo ingeshuhudia pia juu ya Kristo, na yeye aliwahakikishia wanafunzi wake hivi: “Yawafaa ninyi mimi niondoke; kwa maana mimi nisipoondoka, huyo Msaidizi hatakuja kwenu; bali mimi nikienda zangu, nitampeleka kwenu.”—Yohana 14:16, 17, 26; 15:26; 16:7.a
10. Roho takatifu imethibitika kuwa msaidizi katika njia zipi?
10 Kutoka mbinguni, Yesu aliwamwagia wafuasi wake katika siku ya Pentekoste 33 W.K., ile roho takatifu iliyokuwa imeahidiwa. (Matendo 1:4, 5; 2:1-11) Ikiwa msaidizi, roho iliwapa uelewevu wenye kuongezeka juu ya mapenzi na kusudi la Mungu na ikawafungulia Neno lake la kiunabii. (1 Wakorintho 2:10-16; Wakolosai 1:9, 10; Waebrania 9:8-10) Msaidizi huyo pia aliwasaidia wanafunzi wa Yesu wawe mashahidi katika dunia yote. (Luka 24:49; Matendo 1:8; Waefeso 3:5, 6) Leo, roho takatifu yaweza kumsaidia Mkristo aliyejiweka wakfu akue katika maarifa akijifaidi kutokana na maandalizi ya kiroho ambayo Mungu hutoa kupitia “mtumwa mwaminifu mwenye akili.” (Mathayo 24:45-47) Roho ya Mungu yaweza kuandaa msaada kwa kutoa ujasiri na imara inayohitajiwa ili mtu aweze kutoa ushahidi akiwa mmoja wa watumishi wa Yehova. (Mathayo 10:19, 20; Matendo 4:29-31) Hata hivyo, roho takatifu pia husaidia watu wa Mungu katika njia nyinginezo.
-
-
Roho ya Yehova Huwaongoza Watu WakeMnara wa Mlinzi—1992 | Septemba 15
-
-
a Ingawa inapewa hali ya mtu kuwa “msaidizi,” roho takatifu si mtu, kwani kiwakilishi-nafsi cha Kigiriki cha jinsi kati (kinachofasiriwa “it”) hutumiwa kwa roho. Viwakilishi-nafsi vya Kiebrania vya jinsi kike hutumiwa vivyo hivyo kwa hekima inayopewa hali ya mtu. (Mithali 1:20-33; 8:1-36) Isitoshe, roho takatifu ‘ilimwagwa,’ jambo lisiloweza kufanywa kwa mtu.—Matendo 2:33.
-