Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • Kaburi Tupu​—Yesu Yuko Hai!
    Yesu—Njia, Kweli, na Uzima
    • Wale wanawake wanashtuka sana wanapokuta kaburi likiwa tupu! Maria Magdalene anakimbia kwenda kwa “Simoni Petro na yule mwanafunzi mwingine, ambaye Yesu alimpenda,” yaani, mtume Yohana. (Yohana 20:2) Hata hivyo, wale wanawake wengine walio kwenye kaburi wanamwona malaika. Na ndani ya kaburi kuna malaika mwingine, ambaye “amevaa kanzu nyeupe.”—Marko 16:5.

  • Kaburi Tupu​—Yesu Yuko Hai!
    Yesu—Njia, Kweli, na Uzima
    • Kufikia sasa, Maria amewapata Petro na Yohana. Akiwa anahema, anawaambia: “Wamemwondoa Bwana kaburini, nasi hatujui wamemlaza wapi.” (Yohana 20:2) Petro na Yohana wanaondoka mbio. Yohana anakimbia haraka zaidi naye anafika kwenye kaburi kwanza. Anachungulia ndani na kuviona vitambaa, lakini haingii ndani.

      Petro anapofika, anaingia ndani moja kwa moja. Anaona vitambaa vya kitani na kitambaa kilichotumiwa kufunga kichwa cha Yesu. Sasa Yohana anaingia ndani naye anaamini ripoti ya Maria. Licha ya mambo ambayo Yesu alikuwa amesema, hakuna yeyote kati yao anayetambua kwamba amefufuliwa. (Mathayo 16:21) Wanarudi nyumbani wakiwa wamechanganyikiwa. Lakini Maria, ambaye amerudi kwenye kaburi, anabaki hapo.

Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
Toka
Ingia
  • Kiswahili
  • Shiriki
  • Mapendezi
  • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
  • Masharti ya Utumiaji
  • Sera ya Faragha
  • Mpangilio wa Faragha
  • JW.ORG
  • Ingia
Shiriki