Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • Jinsi Fidia Inavyotuokoa
    Mnara wa Mlinzi—2010 | Agosti 15
    • Kuokolewa Kutokana na Ghadhabu ya Mungu

      4, 5. Ni nini kinachothibitisha kwamba ghadhabu ya Mungu inakaa juu ya mfumo huu mwovu wa mambo?

      4 Biblia na mambo hakika ya historia yanaonyesha kwamba tangu Adamu atende dhambi, ghadhabu ya Mungu ‘imekaa juu ya’ jamii ya wanadamu. (Yoh. 3:36) Hilo linaonekana wazi kwa kuwa hakuna mwanadamu ambaye amewahi kuepuka kifo. Utawala wa mpinzani Shetani umeshindwa kabisa kuwalinda wanadamu kutokana na misiba inayoendelea, na hakuna serikali ya kibinadamu ambayo imeweza kuwatimizia raia wake wote mahitaji ya msingi. (1 Yoh. 5:19) Hivyo, wanadamu wanaendelea kuteseka kutokana na vita, uhalifu, na umaskini.

  • Jinsi Fidia Inavyotuokoa
    Mnara wa Mlinzi—2010 | Agosti 15
    • 7 Mtume Paulo alisema kwamba Yesu ‘anatukomboa sisi kutoka kwenye ghadhabu inayokuja.’ (1 The. 1:10) Wonyesho huo wa mwisho wa hasira ya Yehova utasababisha uharibifu wa milele kwa watenda-dhambi wasiotubu. (2 The. 1:6-9) Ni nani atakayeokoka? Biblia inasema hivi: “Yule anayemwamini Mwana ana uzima wa milele; yule asiyemtii Mwana hataona uzima, bali ghadhabu ya Mungu hukaa juu yake.” (Yoh. 3:36) Ndiyo, mfumo huu unapofikia mwisho wake, wote walio hai ambao wanamwamini Yesu na fidia, hawataharibiwa katika siku ya mwisho ya ghadhabu ya Mungu.

Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
Toka
Ingia
  • Kiswahili
  • Shiriki
  • Mapendezi
  • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
  • Masharti ya Utumiaji
  • Sera ya Faragha
  • Mpangilio wa Faragha
  • JW.ORG
  • Ingia
Shiriki