-
Maswali Kutoka kwa WasomajiMnara wa Mlinzi—1988 | Septemba 1
-
-
Angalia yale ambayo Biblia inasema. na yale ambayo kwa kweli haisemi: “Na huko Yerusalemu penye mlango wa kondoo pana birika, iitwayo kwa Kiebrania Bethzatha, nayo ina matao matano [nguzo tano za mfululizo, NW] Ndani ya hayo jamii kubwa ya wagonjwa walikuwa wamelala, vipofu, viwete, nao waliopooza.———Na hapa palikuwa na mtu, ambaye amekuwa hawezi muda wa miaka thelathini na minane. Yesu alipomwona huyu amelala, naye akijua ya kuwa amekuwa hali hiyo siku nyingi, alimwambia, Wataka kuwa mzima? Yule mgonjwa akamjibu, Bwana, mimi sina mtu wa kunitia birikani, maji yanapotibuliwa; ila wakati ninapokuja mimi, mtu mwingine hushuka mbele yangu. Yesu akamwambia, Simama, jitwike godoro lako, uende. Mara yule mtu akawa mzima, akajitwika godoro lake, akaenda.”—Yohana 5:2-9.
-
-
Maswali Kutoka kwa WasomajiMnara wa Mlinzi—1988 | Septemba 1
-
-
Angalia kile kistari-chali kilicho katika nukuu lililo juu la Yohana 5:2-9. Biblia fulani zinatia ndani kifungu cha ziada kinachohesabiwa kuwa Yohana 5:4. Ziada hiyo inasema jambo kama hili “Kwa maana kuna wakati ambapo malaika hushuka, akaingia katika ile birika, akayatibua maji. Basi yeye aliyeingia wa kwanza baada ya maji kutibuliwa, akapona ugonjwa wote uliokuwa umempata.”
Hata hivyo, hesabu fulani ya Biblia za ki-siku-hizi, kutia na New World Translation of the Holy Scriptures, zinaacha nje kifungu hicho. Kwa nini? Kwa sababu yamkini kabisa kifungu hicho hakikuwa katika Gospeli ya Yohana. Maelezo mamoja ya chini katika The Jerusalem Bible yanaonelea kwamba “mashahidi walio bora zaidi” huondoa nje kifungu hicho. “Mashahidi walio bora zaidi” wanaomaamshwa na hati za mkononi za Kigiriki za kale, kama vile Codex Sinaiticus na Vatican 1209 (zote mbili zikiwa ni za karne ya 4 W.K.), na fasiri za mapema katika Kisiriaki na Kilatini Baada ya kutaja ‘kutokuwapo kwa mstari wa 4 katika maandishi ya hati za mkononi zilizo bora zaidi,’ The Expositor’s Bible Commentary inaongezea hivi: “Kwa ujumla hilo linachukuliwa kuwa maelezo la ziada lililoongezewa ili kueleza kusukwa-sukwa kwa maji mara kwa mara, jambo ambalo halaiki ya watu ililichukua kwamba lingeweza kuwa chanzo cha kuponywa.”
Kwa hiyo Biblia haisemi kwa kweli kwamba malaika kutoka kwa Mungu alifanya miujiza kwenye birika la Bethzatha. Basi, je! maponyo ya kimwujiza yalitukia wakati maji yalipotibuliwa? Hakuna mmoja leo anayeweza kusema kwa uhakika. Huenda ikawa pokeo fulani halisitawi kwamba watu wagonjwa sana au walio viwete walikuwa wameponyewa hapo. Hadithi za wenye kusemwa kuwa waliponywa zilipoenea, huenda ikawa watu wenye shida sana walianza kukutana hapo kwa makundi wakitumainia kuponywa. Sisi tunajua kwamba jambo hilo limetukia kwenye sehemu mbalimbali katika wakati wetu, hata wakati ambapo hapana uthibitisho thabiti juu ya maponyo ya kimungu.
-