-
Kutoka Sederi Hadi Kwenye WokovuMnara wa Mlinzi—1990 | Februari 15
-
-
13, 14. Ni jinsi gani damu ya Yesu ni yenye kuokoa uhai na yahitajiwa kabisa kwa wokovu? (Waefeso 1:13)
13 Pia damu yahusika katika wokovu leo—damu ya Yesu iliyomwagwa. “Sikukuu-Kupitwa, msherehekeo wa Wayahudi, ilipokaribia’ katika 32 W.K., Yesu aliwaambia hivi wasikilizaji wengi: “Yeye ambaye ajilisha mnofu wangu na kunywa damu yangu ana uhai wa milele, nami nitafufua yeye kwenye siku ya mwisho; kwa maana mnofu wangu ni chakula cha kweli, na damu yangu ni kinywaji cha kweli.” (Yohana 6:4, 54, 55, NW) Hapo wasikilizaji wake wake Wayahudi wangeifikiria Sikukuu-Kupitwa iliyokuwa inakaribia sana na wangefikiria kwamba damu ya mwana-kondoo ilitumiwa katika Misri.
14 Wakati huo Yesu hakuwa akizungumza juu ya mifano iliyotumiwa katika Mlo wa Jioni wa Bwana. Mwadhimisho mpya huo kwa Wakristo haukuanzishwa mpaka mwaka mmoja baadaye, kwa hiyo hata mitume waliomsikia Yesu katika 32 W.K. hawakuwa na habari kuuhusu. Na bado, Yesu alikuwa anaonyesha kwamba damu yake ilihitajiwa sana kwa wokovu wa milele. Paulo alieleza hivi: “Kwa njia yake sisi tuna uachilio kwa ukombozi kupitia damu ya mmoja huyo, ndiyo, msamaha wa mikiuko yetu, kulingana na mali za fadhili zisizostahiliwa zake.” (Waefeso 1:7, NW) Ni kupitia msamaha tu kwa msingi wa damu ya Yesu kwamba sisi twaweza kuishi milele.
-
-
Kutoka Sederi Hadi Kwenye WokovuMnara wa Mlinzi—1990 | Februari 15
-
-
15. Ni wokovu na mapendeleo gani yaliyokuja kuwezekana kwa Waebrania katika Misri, na ni nini hakikuwezekana? (1 Wakorintho 10:1-5)
15 Uliohusika katika Misri ya kale ulikuwa wokovu wenye mipaka tu. Hakuna mtu aliyeondoka Misri alitarajia kupewa uhai usio na mwisho baada ya huko Kutoka. Ni kweli kwauiba Mungu aliweka Walawi kirasmi wawe makuhani kwa taifa, na baadhi ya kabila la Yuda wakawa wafalme wa kidunia kwa muda, lakini wote hawa wangekufa. (Matendo 2:29; Waebrania 7:11, 23, 27) Ingawa lile “kundi kubwa la watu waliochangamana nao” ambao pia walitoka Misri halikuwa na mapendeleo hayo, wao, pamoja na Waebrania, wangeweza kutumainia kuflkia Bara la Ahadi na kuonea shangwe maisha ya kikawaida huku wakiabudu Mungu. Bado, watumishi wa Yehova wa kabla ya nyakati za Kikristo walikuwa na msingi wa kutumaini kwamba, baada ya muda, wao wangeweza kuuonea shangwe uhai usio na mwisho duniani, ambapo Mungu alikusudia ainabinadamu iishi. Hii ingepatana na ahadi ya Yesu kwenye Yohana 6:54.
16. Watumishi wa kale wangeweza kutumainia wokovu wa namna gani?
16 Mungu alitumia baadhi ya watumishi wake wa kale kuandika maneno ya kuvuvia tumaini kuhusu jambo la kwamba dunia iliumbwa ikaliwe na kwamba wanyofu wangeishi milele juu yayo. (Zaburi 37:9-11; Mithali 2:21, 22; Isaya 45:18) Hata hivyo, waabudu wa kweli wangeweza kupataje wokovu huo wakifa? Kwa kurudishwa na Mungu kwenye uhai duniani. Kwa kielelezo, Ayubu alieleza tumaini la kwamba yeye angekumbukwa na kuitwa arudi kwenye uhai. (Ayubu 14:13-15; Danieli 12:13) Kwa wazi, namna moja ya wokovu ni uhai wa milele duniani.—Mathayo 11:11.
-