Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • Ndugu Zetu na Dada Zetu Ni Akina Nani?
    Jifunze Kutoka kwa Mwalimu Mkuu
    • Je, ndugu za Yesu walikuwa wanafunzi wake pia?— Biblia inasema kwamba mwanzoni ‘hawakumwamini.’ (Yohana 7:5) Hata hivyo, baadaye Yakobo na Yuda wakawa wanafunzi wake, na hata wakaandika vitabu vya Biblia. Unavijua vitabu ambavyo waliandika?— Ndiyo, ni barua ya Yakobo na ya Yuda.

      Tunajua kwamba Yesu alikuwa angalau na dada wawili ijapokuwa hawatajwi katika Biblia. Lakini huenda walikuwa zaidi. Je, dada zake walikuwa wafuasi wake?— Biblia haisemi, kwa hiyo hatujui. Lakini unajua ni kwa nini Yesu aliuliza, “Mama yangu ni nani, na ndugu zangu ni nani?”— Hebu tuone.

  • Ndugu Zetu na Dada Zetu Ni Akina Nani?
    Jifunze Kutoka kwa Mwalimu Mkuu
    • Wakati huo ndugu za Yesu mwenyewe—Yakobo, Yosefu, Simoni, na Yuda—hawakuamini kwamba Yesu ni Mwana wa Mungu. Inaelekea hawakuamini yale ambayo malaika Gabrieli alimwambia mama yao. (Luka 1:30-33) Hivyo, huenda hawakumtendea Yesu kwa fadhili. Yeyote anayefanya hivyo si ndugu au dada wa kweli. Unajua yeyote ambaye hamtendei ndugu yake au dada yake kwa fadhili?—

Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
Toka
Ingia
  • Kiswahili
  • Shiriki
  • Mapendezi
  • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
  • Masharti ya Utumiaji
  • Sera ya Faragha
  • Mpangilio wa Faragha
  • JW.ORG
  • Ingia
Shiriki