Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • Anaelewa Maumivu Yetu
    Mnara wa Mlinzi—2008 | Mei 1
    • Rafiki ya Yesu, Lazaro, alipokufa ghafula, Yesu alienda kwenye kijiji ambacho Lazaro aliishi. Inaeleweka kwa nini dada za Lazaro, Maria na Martha, walilemewa na huzuni. Yesu aliipenda sana familia hiyo. (Yohana 11:5) Basi, angechukua hatua gani? Simulizi linasema hivi: “Yesu alipomwona [Maria] akilia na Wayahudi waliokuja pamoja naye wakilia, akaugua rohoni na kutaabika; naye akasema: ‘Mmemlaza wapi?’ Wakamwambia: ‘Bwana, njoo uone.’ Yesu akatokwa na machozi.” (Yohana 11:33-35) Kwa nini Yesu alilia? Ni kweli kwamba rafiki yake mpendwa Lazaro alikuwa amekufa, lakini muda si muda Yesu angemfufua. (Yohana 11:41-44) Je, kuna jambo lingine lililogusa hisia za Yesu?

      Angalia tena maneno yaliyotajwa juu. Ona kwamba Yesu alipomwona Maria na wale waliokuwa pamoja naye wakilia, ‘aliugua rohoni’ na “kutaabika.” Maneno ya lugha ya awali yaliyotumiwa katika mstari huo yanaonyesha hisia nyingi sana.a Yesu aliguswa moyo sana na mambo aliyoyaona. Hisia nyingi alizokuwa nazo zilionekana wazi alipotokwa na machozi. Kwa wazi, moyo wa Yesu uliguswa na maumivu ya wengine. Je, umewahi kutokwa na machozi kwa sababu mtu fulani unayemjali alikuwa akilia?—Waroma 12:15.

  • Anaelewa Maumivu Yetu
    Mnara wa Mlinzi—2008 | Mei 1
    • a Neno la Kigiriki linalotafsiriwa “akatokwa na machozi” mara nyingi linamaanisha “kulia kimyakimya,” lakini neno linalotumiwa kufafanua kilio cha Maria na cha watu wale wengine linaweza kumaanisha “kulia kwa sauti, kuomboleza.”

Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
Toka
Ingia
  • Kiswahili
  • Shiriki
  • Mapendezi
  • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
  • Masharti ya Utumiaji
  • Sera ya Faragha
  • Mpangilio wa Faragha
  • JW.ORG
  • Ingia
Shiriki