-
“New World Translation” ya Utaalamu na Yenye Kufuatia HakiMnara wa Mlinzi—1991 | Machi 1
-
-
Katika Yohana 1:1 New World Translation yasomeka hivi: “Neno alikuwa mungu.” Katika tafsiri nyingi usemi huo wasomeka hivi tu: “Neno alikuwa Mungu” na unatumiwa kuunga mkono fundisho la Utatu. Haishangazi kwamba wenye kuamini Utatu hawapendi fasiri katika New World Translation. Lakini Yohana 1:1 haikughoshiwa ili kuthibitisha kwamba Yesu si Mungu Mweza Yote. Mashahidi wa Yehova, miongoni mwa wengine wengi, walikuwa wamepinga utumizi wa herufi kubwa katika neno “mungu” muda mrefu kabla New World Translation haijatokea, ambayo hujaribu kufasiri lugha ya kwanza kwa usahihi. Watafsiri Wajerumani watano pia hutumia neno “mungu” katika mstari huo.b Angalau wengine 13 wametumia usemi kama “wa aina ya kimungu” au “aina kama mungu.” Fasiri hizi zinaafikiana na sehemu nyinginezo za Biblia ili kuonyesha kwamba, naam, Yesu mbinguni ni mungu kwa maana ya kuwa wa kimungu. Lakini Yehova na Yesu si mtu mmoja, Mungu yule yule.—Yohana 14:28; 20:17.
-
-
“New World Translation” ya Utaalamu na Yenye Kufuatia HakiMnara wa Mlinzi—1991 | Machi 1
-
-
b Jürgen Becker, Jeremias Felbinger, Oskar Holtzmann, Friedrich Rittelmeyer, na Siegfried Schulz. Emil Bock asema, “mtu wa kimungu.” Ona pia tafsiri za Kiingereza Today’s English Version, The New English Bible, Moffat, Goodspeed.
-