Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • Apolo—Mpiga-Mbiu Mfasaha wa Kweli ya Kikristo
    Mnara wa Mlinzi—1996 | Oktoba 1
    • Mtazamo uleule wa Apolo wa kutojivuna unaonekana wazi pia katika utayari wake wa kukubali barua ya kupendekeza kutoka kwa ndugu Waefeso hadi kwenye kutaniko la Korintho. Simulizi laendelea hivi: “Na alipotaka kuvuka bahari aende mpaka Akaya, ndugu wakamhimiza, wakawaandikia wale wanafunzi wamkaribishe.” (Matendo 18:27; 19:1) Apolo hakudai akubaliwe kwa sababu ya ustahili wake mwenyewe lakini alifuata kwa kiasi mpango wa kutaniko la Kikristo.

  • Apolo—Mpiga-Mbiu Mfasaha wa Kweli ya Kikristo
    Mnara wa Mlinzi—1996 | Oktoba 1
    • Matokeo ya kwanza ya huduma ya Apolo katika Korintho yalikuwa mazuri sana. Kitabu cha Matendo charipoti hivi: “Alipofika akawasaidia sana wale waliokwisha kuamini kwa neema ya Mungu. Kwa maana aliwashinda Wayahudi kabisa kabisa mbele ya watu wote, akionyesha kwa maneno ya maandiko ya kuwa Yesu ni Kristo.”—Matendo 18:27, 28.

      Apolo alijitoa ili kutumikia kutaniko, akiwatia moyo ndugu kwa utayarishaji wake na bidii yake. Ufunguo wa mafanikio yake ulikuwa nini? Kwa hakika Apolo alikuwa na uwezo wa asili na alikuwa na moyo mkuu katika kuvumilia mjadala wa hadharani pamoja na Wayahudi. Lakini la maana zaidi, alisababu kwa kutumia Maandiko.

Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
Toka
Ingia
  • Kiswahili
  • Shiriki
  • Mapendezi
  • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
  • Masharti ya Utumiaji
  • Sera ya Faragha
  • Mpangilio wa Faragha
  • JW.ORG
  • Ingia
Shiriki