Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • Apolo—Mpiga-Mbiu Mfasaha wa Kweli ya Kikristo
    Mnara wa Mlinzi—1996 | Oktoba 1
    • Matokeo ya kwanza ya huduma ya Apolo katika Korintho yalikuwa mazuri sana. Kitabu cha Matendo charipoti hivi: “Alipofika akawasaidia sana wale waliokwisha kuamini kwa neema ya Mungu. Kwa maana aliwashinda Wayahudi kabisa kabisa mbele ya watu wote, akionyesha kwa maneno ya maandiko ya kuwa Yesu ni Kristo.”—Matendo 18:27, 28.

      Apolo alijitoa ili kutumikia kutaniko, akiwatia moyo ndugu kwa utayarishaji wake na bidii yake. Ufunguo wa mafanikio yake ulikuwa nini? Kwa hakika Apolo alikuwa na uwezo wa asili na alikuwa na moyo mkuu katika kuvumilia mjadala wa hadharani pamoja na Wayahudi. Lakini la maana zaidi, alisababu kwa kutumia Maandiko.

  • Apolo—Mpiga-Mbiu Mfasaha wa Kweli ya Kikristo
    Mnara wa Mlinzi—1996 | Oktoba 1
    • Ujumbe uliohubiriwa na Paulo na Apolo ulikuwa uleule, lakini walikuwa na nyutu tofauti. Kwa ukiri wake mwenyewe, Paulo alikuwa “mtu asiyejua kunena”; Apolo, kwa upande mwingine, alikuwa “mfasaha.” (2 Wakorintho 10:10; 11:6) Alikuwa na uwezo mbalimbali uliomwezesha kusikiwa na watu fulani wa jumuiya ya Wayahudi katika Korintho. Alifanikiwa katika ‘kuwashinda Wayahudi kabisa kabisa,’ hali Paulo alikuwa ameliondoka sinagogi, muda mfupi uliopita.—Matendo 18:1, 4-6.

Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
Toka
Ingia
  • Kiswahili
  • Shiriki
  • Mapendezi
  • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
  • Masharti ya Utumiaji
  • Sera ya Faragha
  • Mpangilio wa Faragha
  • JW.ORG
  • Ingia
Shiriki