Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • “Mapenzi ya Yehova na Yatendeke”
    “Kutoa Ushahidi Kamili” Kuhusu Ufalme wa Mungu
    • Matendo 21:1-17

      1-4. Kwa nini Paulo anaenda Yerusalemu, na nini kinachomngojea huko?

      WATU wengi wamehuzunika baada ya Paulo kuondoka huko Mileto. Si rahisi kwa Paulo na Luka kuachana na wazee wa Efeso, waliowapenda sana! Wamishonari hao wawili wamesimama kwenye sitaha. Mizigo yao ina vitu wanavyohitaji kwa ajili ya safari. Pia wamebeba michango iliyokusanywa kwa ajili ya Wakristo wenye uhitaji huko Yudea nao wanakusudia kuwasilisha salama zawadi hizo.

      2 Upepo mwanana unajaza matanga na meli yang’oa nanga. Wanaume hao wawili, na wengine saba wanaosafiri pamoja nao, wanawatazama ndugu zao wenye huzuni waliobaki ufuoni. (Mdo. 20:4, 14, 15) Wasafiri hao wanaendelea kupunga mikono mpaka wanapokuwa mbali wasiweze tena kuwaona rafiki zao.

  • “Mapenzi ya Yehova na Yatendeke”
    “Kutoa Ushahidi Kamili” Kuhusu Ufalme wa Mungu
    • 5. Paulo na wenzake walipitia njia gani kwenda Tiro?

      5 Meli ambayo Paulo na wenzake walipanda ‘ilienda moja kwa moja.’ Hilo linamaanisha kwamba kulikuwa na upepo mzuri uliovuma, na meli haikushusha matanga hadi walipofika Kosi siku hiyo. (Mdo. 21:1) Inaonekana kwamba meli hiyo ilitia nanga huko usiku kucha kabla ya kuelekea Rode na Patara. Walipofika Patara, katika pwani ya kusini ya Asia Ndogo, ndugu hao walipanda meli kubwa ya shehena, iliyowapeleka moja kwa moja hadi Tiro, Foinike. Wakiwa njiani, walikiacha nyuma “kisiwa cha Kipro . . . upande wa kushoto.” (Mdo. 21:3) Kwa nini Luka, aliyeandika kitabu cha Matendo, anataja jambo hilo?

Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
Toka
Ingia
  • Kiswahili
  • Shiriki
  • Mapendezi
  • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
  • Masharti ya Utumiaji
  • Sera ya Faragha
  • Mpangilio wa Faragha
  • JW.ORG
  • Ingia
Shiriki