Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • “Nisikilizeni Ninapojitetea”
    “Kutoa Ushahidi Kamili” Kuhusu Ufalme wa Mungu
    • 11. Wazee walimwagiza Paulo afanye nini, na huenda ni nini kilichohusika? (Ona pia maelezo ya chini.)

      11 Ijapokuwa uvumi uliokuwa umeenea haukuwa wa kweli, bado uliwasumbua waamini Wayahudi. Ndiyo sababu wazee walimwagiza Paulo: “Tuna wanaume wanne waliojiwekea nadhiri. Nenda pamoja na watu hawa ukajitakase kisherehe pamoja nao na kuwagharimia, ili wanyolewe vichwa vyao. Ndipo kila mtu atajua kwamba uvumi walioambiwa kukuhusu si wa kweli, bali unatembea kwa utaratibu, na pia unashika Sheria.”c—Mdo. 21:23, 24.

      12. Paulo alionyeshaje kwamba alikuwa tayari kubadilika kulingana na hali na kufuata maagizo ya wazee wa Yerusalemu?

      12 Paulo angeweza kushikilia msimamo wake na kudai kwamba tatizo si uvumi ulioenea kumhusu, bali ni maoni ya waamini hao Wayahudi kuhusu Sheria ya Musa. Badala ya kufanya hivyo, alikuwa tayari kubadilika kulingana na hali maadamu kufanya hivyo hakungevunja viwango vya Mungu. Mapema alikuwa ameandika hivi: “Kwa wale walio chini ya sheria nilikuwa kama aliye chini ya sheria, ingawa mimi mwenyewe siko chini ya sheria, ili niwapate wale walio chini ya sheria.” (1 Kor. 9:20) Katika kisa hiki, Paulo aliamua kufuata maagizo ya wazee wa Yerusalemu na kuwa “kama aliye chini ya sheria.” Kwa kufanya hivyo, alituwekea kielelezo kizuri cha kufuata maagizo ya wazee badala ya kuamua kufanya mambo kwa njia yetu.​—Ebr. 13:17.

      Picha: 1. Paulo akisikiliza mwongozo wa wazee wa Yerusalemu. 2. Mkutano wa wazee katika siku zetu, ndugu akifikiria kwa makini wazee wengine wanaponyoosha mikono.

      Ikiwa hakuna kanuni za Kimaandiko zilizohusika, Paulo alikuwa tayari kubadilika kulingana na hali. Je, wewe hufanya hivyo?

      SHERIA YA WAROMA NA RAIA WA ROMA

      Kwa kawaida serikali ya Roma haikuingilia mambo ya serikali za mikoa. Kwa ujumla Wayahudi walikuwa na sheria zao. Waroma waliingilia kesi ya Paulo kwa sababu ghasia zilizotokea zingeweza kuvuruga amani.

      Watawala wa Roma walikuwa na mamlaka kubwa juu ya watu wengine waliokuwa wakiishi katika mikoa ya Roma ambao hawakuwa raia wa Roma. Hata hivyo, wenye mamlaka walishughulika kwa njia tofauti na raia wa Roma.f Kuwa raia wa Roma kulimpa mtu haki na uhuru fulani ulioheshimiwa katika milki hiyo yote. Kwa mfano, ilikuwa kinyume cha sheria kwa mtu kumfunga au kumpiga Mroma yeyote ambaye hajahukumiwa hatia, kwa sababu watumwa tu ndio waliotendewa hivyo. Pia, Waroma walikuwa na haki ya kukata rufani kwa maliki aliye Roma dhidi ya uamuzi uliofanywa na mtawala wa mkoa.

      Uraia wa Roma ungeweza kupatikana kwa njia mbalimbali. Kwanza, kupitia urithi. Mara chache Maliki mbalimbali waliwapatia uraia watu au wakaaji wa majiji au wilaya nzima kwa sababu ya huduma zao. Mtumwa aliyenunua uhuru wake kutoka kwa raia wa Roma, mtumwa aliyewekwa huru na Mroma, au askari asiye Mroma ambaye aliachishwa kazi kutoka katika jeshi la Roma angeweza kuwa raia wa Roma. Inaonekana katika hali fulani ingewezekana kununua uraia. Ndiyo sababu kiongozi wa kijeshi Klaudio Lisia alimwambia hivi Paulo: “Mimi nilinunua haki hizo za kuwa raia kwa pesa nyingi.” Paulo akasema: “Lakini mimi nina haki hizo kwa kuzaliwa.” (Mdo. 22:28) Hivyo, inawezekana kwamba mmoja wa babu za Paulo alipata uraia wa Roma, ingawa hakuna uthibitisho.

      f Katika karne ya kwanza W.K., hakukuwa na Waroma wengi katika mkoa wa Yudea. Kuanzia karne ya tatu ndipo watu waliokuwa wakiishi katika mikoa ya Roma walianza kupewa uraia.

  • “Nisikilizeni Ninapojitetea”
    “Kutoa Ushahidi Kamili” Kuhusu Ufalme wa Mungu
    • c Wasomi fulani wanadokeza kwamba watu hao walikuwa wameweka Nadhiri. (Hes. 6:1-21) Ni kweli kwamba Sheria ya Musa, iliyotumika kuweka nadhiri hizo, haikuwa ikitumika tena. Hata hivyo, huenda Paulo aliona kwamba hakuna ubaya kwa watu hao kutimiza nadhiri waliyoweka kwa Yehova. Kwa hiyo, haingekuwa vibaya kulipa gharama zao na kuandamana nao. Hatujui ni nadhiri ya aina gani iliyowekwa, hata hivyo, haielekei kwamba Paulo angeshiriki kutoa dhabihu ya mnyama (kama Wanadhiri walivyofanya), akiamini kwamba ingesafisha dhambi za mtu. Dhabihu kamilifu ya Kristo ilikuwa imeondolea mbali uwezo wa dhabihu hizo kusafisha dhambi. Vyovyote vile, tuna hakika kwamba Paulo hangekubali kufanya chochote ambacho kingechafua dhamiri yake.

Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
Toka
Ingia
  • Kiswahili
  • Shiriki
  • Mapendezi
  • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
  • Masharti ya Utumiaji
  • Sera ya Faragha
  • Mpangilio wa Faragha
  • JW.ORG
  • Ingia
Shiriki