Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • “Mimi Nakata Rufani kwa Kaisari!”
    Mnara wa Mlinzi—2001 | Desemba 15
    • KIKUNDI cha wafanya-ghasia chamkamata mtu fulani asiyeweza kujitetea na kuanza kumpiga. Wafanya-ghasia hao wafikiri kwamba mtu huyo anastahili kuuawa. Wakati tu inapoonekana kwamba mtu huyo atauawa na wafanya-ghasia hao wenye jeuri, askari watokea na wajitahidi sana kumwokoa mtu huyo. Mtu huyo ni mtume Paulo. Wafanya-ghasia hao wanaomshambulia ni Wayahudi ambao wanapinga vikali mahubiri ya Paulo na kumshtumu kwamba anatia hekalu unajisi. Watu wanaomwokoa ni Waroma, wakiongozwa na kamanda wao, Klaudio Lisiasi. Katika vurugu hiyo, Paulo anakamatwa kwa kushukiwa kuwa mtenda-maovu.

      Sura saba za mwisho za kitabu cha Matendo zaonyesha kesi iliyoanza baada ya kukamatwa huko. Kuelewa malezi ya Paulo, mashtaka aliyofanyiwa, jinsi alivyojitetea, na jinsi Waroma walivyotoa adhabu kutatusaidia kuelewa sura hizo zaidi.

  • “Mimi Nakata Rufani kwa Kaisari!”
    Mnara wa Mlinzi—2001 | Desemba 15
    • Baadhi ya majukumu ya Klaudio Lisiasi yalitia ndani kudumisha amani jijini Yerusalemu. Mkubwa wa Lisiasi, gavana Mroma wa Yudea, aliishi Kaisaria. Hatua aliyochukua Lisiasi kuhusiana na Paulo yaonyesha kwamba alitaka kumlinda Paulo na pia kumweka kizuizini mtu aliyekuwa anavuruga amani. Kwa sababu ya itikio la Wayahudi, Lisiasi alimpeleka mfungwa wake kwenye kambi ya askari katika Mnara wa Antonia.—Matendo 21:27–22:24.

Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
Toka
Ingia
  • Kiswahili
  • Shiriki
  • Mapendezi
  • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
  • Masharti ya Utumiaji
  • Sera ya Faragha
  • Mpangilio wa Faragha
  • JW.ORG
  • Ingia
Shiriki