Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • Kuomba Msamaha—Ni Njia Bora ya Kufanya Amani
    Mnara wa Mlinzi—2002 | Novemba 1
    • Mtume Paulo pia alijua wakati wa kuomba msamaha. Pindi moja ilimbidi ajitetee mbele ya Sanhedrini, mahakama kuu ya Wayahudi. Kuhani mkuu Anania alikasirishwa sana na maneno ya unyofu ya Paulo hivyo akawaagiza wale waliokuwa wamesimama karibu naye wampige mdomoni. Ndipo Paulo akamwambia: “Mungu atakupiga wewe, ewe ukuta uliopakwa chokaa. Je, wakati uleule mmoja waketi kunihukumu kupatana na Sheria na, kwa kukiuka Sheria, waamuru nipigwe?” Watazamaji walipomshutumu Paulo kwa kumtukana kuhani wa cheo cha juu, mtume huyo alikubali kosa lake mara moja na kusema: “Akina ndugu, sikujua yeye ni kuhani wa cheo cha juu. Kwa maana imeandikwa, ‘Wewe hupaswi kusema vibaya juu ya mtawala wa watu wako.’”—Matendo 23:1-5.

      Maneno ya Paulo—kwamba yule aliyekuwa amewekwa kuwa hakimu hapaswi kutumia jeuri—ni ya kweli. Hata hivyo, aliomba msamaha kwa kuwa bila kujua alizungumza na kuhani wa cheo cha juu kwa njia ambayo ingeweza kuonekana kuwa yenye kukosa heshima.a Kwa sababu Paulo aliomba msamaha, Sanhedrini ilimsikiliza. Kwa kuwa Paulo alijua mabishano yaliyokuweko kati ya washiriki wa mahakama hiyo, aliwaambia kwamba alikuwa ameshtakiwa kwa sababu aliamini ufufuo. Hivyo, mgawanyiko mkubwa ukatokea, huku Mafarisayo wakimwunga mkono Paulo.—Matendo 23:6-10.

  • Kuomba Msamaha—Ni Njia Bora ya Kufanya Amani
    Mnara wa Mlinzi—2002 | Novemba 1
    • a Huenda Paulo hakumtambua kuhani huyo wa cheo cha juu kwa sababu hakuwa anaona vizuri.

Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
Toka
Ingia
  • Kiswahili
  • Shiriki
  • Mapendezi
  • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
  • Masharti ya Utumiaji
  • Sera ya Faragha
  • Mpangilio wa Faragha
  • JW.ORG
  • Ingia
Shiriki