Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • “Mimi Nakata Rufani kwa Kaisari!”
    Mnara wa Mlinzi—2001 | Desemba 15
    • Paulo alijitetea kwa kuzungumzia hoja moja baada ya nyingine. ‘Sijasababisha usumbufu wowote. Ni kweli kwamba mimi ni mshiriki wa “farakano” kama wanavyoliita, lakini kuwa mshiriki wa farakano huonyesha kwamba mtu anafuata sheria za Wayahudi. Wayahudi fulani wa Asia ndio waliochochea ghasia hizo. Ikiwa wana malalamiko, wanapaswa kuja hapa na kuyataja.’ Kwa kweli Paulo alionyesha kwamba mashtaka hayo hayakuwa ya kisiasa bali ni mzozo tu wa kidini miongoni mwa Wayahudi, ambao Roma haingeweza kufanya chochote kuuhusu. Huku akiwa mwenye hadhari asiwaudhi Wayahudi wasiopenda kutawaliwa, Feliksi aliahirisha uamuzi huo wa mahakama na hivyo hakuna hatua yoyote ambayo ingeweza kuchukuliwa. Paulo hakukabidhiwa kwa Wayahudi waliodai kuwa na uwezo wa kuhukumu, wala hakuhukumiwa kwa Sheria ya Roma, wala hakuachiliwa. Feliksi hangelazimishwa kutoa hukumu, na mbali na kutaka kuwapendeza Wayahudi, alikuwa na sababu nyingine ya kuchelewesha mambo—alifikiri kwamba Paulo angemhonga.—Matendo 24:10-19, 26.b

  • “Mimi Nakata Rufani kwa Kaisari!”
    Mnara wa Mlinzi—2001 | Desemba 15
    • b Bila shaka jambo hilo lilikuwa kinyume cha sheria. Kichapo kimoja chasema hivi: “Chini ya sheria inayohusu kutoza pesa kwa nguvu, Lex Repetundarum, mtu yeyote aliyekuwa na mamlaka au usimamizi fulani hakuruhusiwa kuomba au kukubali hongo ili kumfunga au kumfungua mtu, kumhukumu au kutomhukumu au kumwachilia mfungwa.”

Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
Toka
Ingia
  • Kiswahili
  • Shiriki
  • Mapendezi
  • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
  • Masharti ya Utumiaji
  • Sera ya Faragha
  • Mpangilio wa Faragha
  • JW.ORG
  • Ingia
Shiriki