Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • Kwa Nini Sauli Alinyanyasa Wakristo?
    Mnara wa Mlinzi—1999 | Juni 15
    • Damaski lilikuwa umbali wa kilometa 220 hivi—safari ya siku saba au nane kwa miguu—kutoka Yerusalemu. Hata hivyo, “akipumua tisho na uuaji-kimakusudi dhidi ya wanafunzi,” Sauli alienda kwa kuhani wa cheo cha juu na kumwomba barua za kwenda kwenye masinagogi huko Damaski. Kufanya nini? Ili apate kuwaleta hadi Yerusalemu wakiwa wamefungwa wowote ambao angewapata walio wa “Ile Njia.” Akiwa ameidhinishwa rasmi, Sauli ‘alianza kushughulikia kutaniko kwa njia mbaya kabisa akivamia nyumba moja baada ya nyingine, akikokota nje wanaume na pia wanawake, akawa akiwakabidhi gerezani.’ Wengine ‘akawapiga viboko katika sinagogi,’ naye ‘akaitupa kura yake’ (kihalisi, ‘jiwe lake la mviringo la kupigia kura’) kutaka wauawe.—Matendo 8:3; 9:1, 2, 14; 22:5, 19; 26:10, kielezi-chini katika New World Translation—With References.

      Kwa kuzingatia yale ambayo Sauli alifunzwa na Gamalieli na uwezo aliokuwa nao sasa, wasomi fulani wanaamini kwamba Sauli alikuwa amefanya maendeleo kutoka kuwa mwanafunzi tu wa Sheria hadi kufikia kiwango cha kuwa na mamlaka ya kiasi fulani katika Dini ya Wayahudi. Kwa mfano, mmoja alidai kwamba inawezekana kwamba Sauli alikuwa mwalimu katika sinagogi fulani Yerusalemu. Hata hivyo, ni nini kimaanishwacho na Sauli ‘kutupa kura yake’—awe alikuwa mshiriki wa mahakama au mtu aliyeunga mkono kuuawa kwa Wakristo—hatuwezi kuwa na uhakika.a

  • Kwa Nini Sauli Alinyanyasa Wakristo?
    Mnara wa Mlinzi—1999 | Juni 15
    • a Kulingana na kitabu The History of the Jewish People in the Age of Jesus Christ (175 B.C.–A.D. 135), cha Emil Schürer, ingawa Mishnah haielezi chochote kuhusu taratibu za Sanhedrini Kuu, au Sanhedrini yenye Watu Sabini na Mmoja, taratibu za zile Sanhedrini ndogo, zenye watu 23, zimeelezwa kinaganaga. Wanafunzi wa sheria wangeweza kuhudhuria kesi za mauaji zilizoshughulikiwa na Sanhedrini ndogo, ambapo waliruhusiwa kumtetea mshtakiwa wala si kusema dhidi yake. Katika kesi zisizohusisha kosa la mauaji, wangeweza kufanya yote hayo.

Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
Toka
Ingia
  • Kiswahili
  • Shiriki
  • Mapendezi
  • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
  • Masharti ya Utumiaji
  • Sera ya Faragha
  • Mpangilio wa Faragha
  • JW.ORG
  • Ingia
Shiriki