Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • Filipo Ambatiza Ofisa Mwethiopia
    Mnara wa Mlinzi—1996 | Julai 15
    • HUKU akisafiri kwa gari lake, Mwethiopia alikuwa akiutumia wakati wake kwa hekima. Alikuwa akisoma kwa sauti—zoea la kawaida miongoni mwa wasafiri wa karne ya kwanza. Mtu huyo mahususi alikuwa ofisa “mwenye mamlaka chini ya Kandake malkia wa Kushi.”a Alikuwa “juu ya hazina yake yote”—kihalisi, alikuwa waziri wa fedha. Ofisa huyo alikuwa akisoma Neno la Mungu ili apate ujuzi.—Matendo 8:27, 28.

  • Filipo Ambatiza Ofisa Mwethiopia
    Mnara wa Mlinzi—1996 | Julai 15
    • a “Kandake” si jina bali ni jina la cheo (sawa na “Farao” na “Kaisari”) lililotumiwa kwa mfuatano wa malkia mbalimbali wa Ethiopia.

  • Filipo Ambatiza Ofisa Mwethiopia
    Mnara wa Mlinzi—1996 | Julai 15
    • Kwa Nini Aliitwa Towashi?

      Kotekote katika simulizi la Matendo sura ya 8, yule Mwethiopia anarejezewa kuwa “towashi.” Hata hivyo, kwa kuwa Sheria ya Kimusa haikuruhusu mwanamume aliyehasiwa kuingia katika kutaniko, ni wazi kwamba mwanamume huyo hakuwa towashi katika maana halisi. (Kumbukumbu la Torati 23:1) Neno “towashi” katika Kigiriki laweza kutumiwa kwa mtu aliye na cheo cha juu. Kwa njia hiyo, huyo Mwethiopia alikuwa ofisa chini ya yule malkia wa Ethiopia.

Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
Toka
Ingia
  • Kiswahili
  • Shiriki
  • Mapendezi
  • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
  • Masharti ya Utumiaji
  • Sera ya Faragha
  • Mpangilio wa Faragha
  • JW.ORG
  • Ingia
Shiriki