Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • Ubatizo
    Ufahamu wa Kina wa Maandiko
    • Kwa habari ya Wayahudi, agano la Sheria lilifutiliwa mbali kwa msingi wa kifo cha Kristo juu ya mti wa mateso (Kol 2:14), na agano jipya lilianza kutenda kazi katika Pentekoste, 33 W.K. (Linganisha Mdo 2:4; Ebr 2:3, 4.) Hata hivyo, Mungu alirefusha kipindi cha kibali cha pekee kwa Wayahudi kwa karibu miaka mitatu na nusu zaidi. Wakati huo wanafunzi wa Yesu walifanya mahubiri yao kwa Wayahudi, watu waliogeuza imani ikawa ya Kiyahudi, na Wasamaria. Lakini karibu mwaka 36 W.K. Mungu alimwelekeza Petro aende nyumbani kwa Kornelio Mtu wa Mataifa, ofisa wa jeshi Mroma, na kwa kumimina roho Yake takatifu juu ya Kornelio na nyumba yake, akamwonyesha Petro kwamba Watu wa Mataifa wangeweza sasa kukubaliwa wabatizwe kwa maji. (Mdo 10:34, 35, 44-48) Kwa kuwa sasa Mungu hakulitambua tena lile agano la Sheria pamoja na Wayahudi waliotahiriwa ila sasa alitambua tu agano lake jipya lililopatanishwa na Yesu Kristo, Wayahudi wa asili, wawe wametahiriwa au hawajatahiriwa, hawakuonwa na Mungu kuwa wamo katika uhusiano wowote wa pekee pamoja naye. Hawangeweza kupata kibali cha Mungu kwa kushika Sheria hiyo, ambayo haikuwa na uhalali tena, wala kupitia ubatizo wa Yohana, uliohusiana na ile Sheria, bali waliwajibika kumfikia Mungu kupitia imani katika Mwanaye na kubatizwa katika maji katika jina la Yesu Kristo ili watambuliwe na kupata kibali cha Yehova.—Ona MAJUMA SABINI (Agano kutendeshwa “kwa juma moja”).

  • Ubatizo
    Ufahamu wa Kina wa Maandiko
    • Hakuna Ubatizo wa Watoto Wachanga. Kwa kuwa ‘kusikia neno,’ ‘kulikubali neno kwa ukunjufu wa moyo,’ na ‘kutubu’ hutangulia ubatizo wa maji (Mdo 2:14, 22, 38, 41) na kwa kuwa ubatizo hutaka mtu afanye uamuzi mzito, ni wazi kwamba ni lazima mtu awe na umri wa kutosha ili asikie, asadiki, na kufanya uamuzi huo. Hoja fulani hutolewa na wengine kuunga mkono ubatizo wa watoto wachanga. Wao hurejezea visa ambavyo katika hivyo ‘watu wa nyumba’ fulani-fulani walibatizwa, kama vile watu wa nyumba ya Kornelio, Lidia, yule mlinzi wa jela Mfilipi, Krispo, na Stefana. (Mdo 10:48; 11:14; 16:15, 32-34; 18:8; 1Ko 1:16) Wanasadiki kwamba hilo ladokeza kuwa watoto wachanga katika familia hizo walibatizwa pia. Lakini, katika kisa cha Kornelio, wale waliobatizwa walikuwa ni ambao walikuwa wamelisikia neno na kupokea roho takatifu, nao walisema katika lugha na kumtukuza Mungu; mambo hayo hayangeweza kutumika kuhusiana na watoto wachanga. (Mdo 10:44-46) Lidia alikuwa “mwabudu wa Mungu, . . . na Yehova akafungua wazi moyo wake asikilize kwa makini mambo yaliyokuwa yakisemwa na Paulo.” (Mdo 16:14) Ilimbidi yule mlinzi wa jela Mfilipi ‘amwamini Bwana Yesu,’ na hilo ladokeza kwamba wengine katika familia yake walipaswa pia kuamini ili wabatizwe. (Mdo 16:31-34) “Krispo ofisa-msimamizi wa sinagogi akawa mwamini katika Bwana, na ndivyo na watu wote wa nyumba yake.” (Mdo 18:8) Hayo yote yanadhihirisha kwamba kuhusiana na ubatizo kulikuwa mambo kama vile kusikia, kuamini, na kumtukuza Mungu, mambo ambayo watoto wachanga hawawezi kufanya. Huko Samaria waliposikia na kuamini “habari njema ya ufalme wa Mungu na juu ya jina la Yesu Kristo, wakabatizwa.” Hapa Maandiko yanaonyesha kihususa kwamba watu waliobatizwa hawakuwa watoto wachanga, bali “wanaume na pia wanawake.”—Mdo 8:12.

Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
Toka
Ingia
  • Kiswahili
  • Shiriki
  • Mapendezi
  • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
  • Masharti ya Utumiaji
  • Sera ya Faragha
  • Mpangilio wa Faragha
  • JW.ORG
  • Ingia
Shiriki