Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • “Kujawa na Shangwe na Roho Takatifu”
    “Kutoa Ushahidi Kamili” Kuhusu Ufalme wa Mungu
    • 5. Eleza jinsi kisiwa cha Kipro kilivyohubiriwa.

      5 Baada ya kutembea hadi Seleukia, bandari iliyokuwa karibu na Antiokia, Barnaba na Sauli walisafiri kwa mashua hadi kisiwa cha Kipro, umbali wa kilomita 200 hivi.d Kwa kuwa alikuwa mzaliwa wa Kipro, bila shaka Barnaba alikuwa na hamu kubwa ya kutangaza habari njema katika eneo la nyumbani kwao. Walipofika Salami, jiji lililokuwa kwenye ufuo wa mashariki wa kisiwa hicho, wanaume hao hawakupoteza wakati wowote. Mara moja, “wakaanza kulitangaza neno la Mungu katika masinagogi ya Wayahudi.”e (Mdo. 13:5) Barnaba na Sauli walisafiri kutoka upande mmoja hadi upande wa pili wa Kipro, wakihubiri katika majiji makubwa yaliyokuwa njiani. Ikitegemea barabara waliyopitia, huenda wamishonari hao walitembea kilomita 160 hivi!

      MASINAGOGI YA WAYAHUDI

      Neno “sinagogi” linamaanisha “kukusanya pamoja.” Mwanzoni, neno hilo lilimaanisha kusanyiko au kutaniko la Wayahudi na baadaye likapata maana mpya yaani mahali au jengo lililotumiwa kwa ajili ya kusanyiko hilo.

      Inaaminika kwamba masinagogi yalianza kutumiwa wakati wa ile miaka 70 Wayahudi walipokuwa uhamishoni Babiloni au muda mfupi baada ya kutoka huko. Masinagogi yalikuwa mahali pa kutoa elimu, kuabudu, kusoma na kufafanua Maandiko, na kuchochea watu kiroho. Katika karne ya kwanza W.K., kila mji katika maeneo ya Palestina ulikuwa na sinagogi. Majiji makubwa, kama Yerusalemu, yalikuwa na masinagogi kadhaa.

      Hata hivyo, si Wayahudi wote waliorudi Palestina baada ya uhamisho wa Babiloni. Wengi walihamia nchi nyingine ili kufanya biashara. Kufikia karne ya tano hivi K.W.K., Wayahudi walikuwa wakiishi katika wilaya zote 127 za Milki ya Uajemi. (Esta 1:1; 3:8) Baada ya muda, wakaanza kuishi katika majiji yaliyozunguka Bahari ya Mediterania. Wayahudi hao walioishi katika maeneo hayo wakaanza kujenga masinagogi.

      Katika masinagogi, Sheria ilisomwa na kufafanuliwa kila Sabato. Kulikuwa na jukwaa la kusomea lililozungukwa na viti katika pande tatu. Mwanamume yeyote Myahudi aliyekuwa mwamini angeweza kusoma, kuhubiri, au kuwahimiza wengine katika sinagogi.

  • “Kujawa na Shangwe na Roho Takatifu”
    “Kutoa Ushahidi Kamili” Kuhusu Ufalme wa Mungu
    • d Katika karne ya kwanza, meli zingeweza kusafiri kilomita 150 hivi kwa siku ikitegemea upepo. Safari hiyo ingechukua muda mrefu zaidi ikiwa hali ya hewa ni mbaya.

Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
Toka
Ingia
  • Kiswahili
  • Shiriki
  • Mapendezi
  • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
  • Masharti ya Utumiaji
  • Sera ya Faragha
  • Mpangilio wa Faragha
  • JW.ORG
  • Ingia
Shiriki