-
Damu—Ni Muhimu kwa UhaiDamu Yaweza Kuokoaje Uhai Wako?
-
-
Angalia ilivyotukia wakati, miaka mingi baada ya kifo cha Yesu, swali lilipozuka juu ya kama mtu anayekuwa Mkristo angelazimika kushika sheria zote za Israeli. Jambo hilo lilizungumzwa kwenye mkutano wa baraza lenye kuongoza la Kikristo, ambalo lilitia ndani mitume. Yakobo ndugu-nusu wa Yesu alirejezea maandishi yaliyokuwa na amri juu ya damu ambazo alitaarifiwa Noa na taifa la Israeli. Je! amri hizo zingetumika kwa Wakristo?—Matendo 15:1-21.
Baraza hilo lilipelekea makundi yote uamuzi wao: Wakristo hawakuhitaji kushika fungu la sheria alilopewa Musa, lakini ilikuwa “lazima” kwao ‘wajiepushe na vitu vilivyotolewa sadaka kwa sanamu, na damu, na nyama zilizosongolewa [nyama zisizoondolewa damu], na uasherati.’ (Matendo 15:22-29) Mitume hawakuwa wakitoa kawaida tu za kidini au amri ya ulaji. Amri hiyo iliweka kawaida za msingi za elimu ya maadili, ambazo Wakristo wa mapema walitii. Wapata mwongo mmoja baadaye walikiri kwamba wangali wapaswa ‘wajilinde nafsi zao na vitu vilivyotolewa sadaka kwa sanamu, na damu, na kitu kilichosongolewa, na uasherati.’—Matendo 21:25.
Wewe unajua kwamba mamilioni ya watu huhudhuria makanisa. Pengine walio wengi wao wangekubali kwamba elimu ya maadili ya Kikristo inahusu kutoipa mifano ibada wala kushiriki katika ukosefu mbaya sana wa adili. Hata hivyo, tunastahili kuangalia kwamba mitume waliweka kujiepusha na damu katika kiwango kile kile cha kiadili kama vile kujiepusha na makosa hayo. Uamuzi wao ulimalizia hivi: “Ikiwa kwa uangalifu nyinyi mnajiepusha wenyewe na vitu hivyo, nyinyi mtafanikiwa. Afya njema kwenu nyinyi!”—Matendo 15:29, NW.
Uamuzi wa kimitume ulieleweka kwa muda mrefu kuwa ulikuwa ungali watumika. Eusebio asimulia juu ya mwanamke mmoja kijana karibu na mwisho wa karne ya pili, ambaye kabla ya kufa chini ya mateso, alikazia jambo la kwamba Wakristo “hawaruhusiwi kula damu hata ya wanyama wasiofikiri.” Yeye hakuwa akitumia haki yake ya kufa. Alitaka kuishi, lakini yeye hangeridhiana juu ya kanuni zake. Je! wewe hustahi wale ambao huweka kanuni juu ya pato la kibinafsi.
Mwanasayansi Joseph Priestley alifikia mkataa huu: “Katazo la kutokula damu, alilopewa Noa, laonekana kuwa lenye kutumika kwa uzao wake wote . . . Tukifasiri [lile] katazo la mitume kwa zoea la Wakristo wa kwanza, ambao hawawezi kudhaniwa ifaavyo hata kidogo kwamba hawakuelewa asili na kadiri yalo, hatuwezi kufanya lolote ila kukata kauli, kwamba lilikusudiwa liwe kamili na la muda wote; kwa kuwa damu haikuliwa na Wakristo wowote kwa karne nyingi.”
-
-
Damu—Ni Muhimu kwa UhaiDamu Yaweza Kuokoaje Uhai Wako?
-
-
[Sanduku katika ukurasa wa 4]
‘‘Mawazo yaliyoandikwa hapa kwa njia ya utaratibu na barabara [katika Matendo 15] yanastahilishwa kuwa ya lazima, yakitoa ithibati yenye nguvu zaidi kwamba katika akili za mitume huo haukuwa mpango wa kitambo, au hatua ya muda tu.” — Profesa Édouard Reuss, Chuo Kikuu cha Strasbourg.
-