Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • Via Egnatia—Barabara Kuu Iliyosaidia Kuleta Mpanuko
    Amkeni!—1997 | Agosti 22
    • Msaada mkubwa sana katika kueneza Ukristo katika Makedonia ulikuwa Via Egnatia, barabara kuu ya Roma iliyotengenezwa. Baada ya kutua kwenye bandari ya Neapolisi (sasa Kaválla, Ugiriki) mwisho wa kaskazini mwa Bahari ya Aegean, wamishonari hao kwa wazi walisafiri kwenye barabara kuu hiyo hadi Filipi, jiji kuu la wilaya ya Makedonia. Barabara hiyo iliendelea hadi Amfipolisi, Apolonia, na Thesalonike, zilizokuwa sehemu ambazo Paulo angetua pamoja na waandamani wake.—Matendo 16:11–17:1.

  • Via Egnatia—Barabara Kuu Iliyosaidia Kuleta Mpanuko
    Amkeni!—1997 | Agosti 22
    • Hata hivyo, Via Egnatia, ililetea watu wengi walioishi katika eneo hilo manufaa kuu zaidi kuliko ufanisi wa kimwili. Kwa mfano, chukua mfanya-biashara mwanamke mwenye ufanisi Lidia. Yeye aliishi Filipi—jiji la kwanza katika Ulaya kusikia Paulo akihubiri habari njema. Baada ya kutua Neapolisi katika mwaka wa 50 W.K., mtume Paulo na waandamani wake walisafiri kilometa 16 kuelekea kaskazini-magharibi kwenye Via Egnatia hadi Filipi.

Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
Toka
Ingia
  • Kiswahili
  • Shiriki
  • Mapendezi
  • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
  • Masharti ya Utumiaji
  • Sera ya Faragha
  • Mpangilio wa Faragha
  • JW.ORG
  • Ingia
Shiriki