-
“Vuka Uingie Makedonia”“Kutoa Ushahidi Kamili” Kuhusu Ufalme wa Mungu
-
-
16. Ni nini kilichotokea siku moja baada ya Paulo na Sila kupigwa viboko?
16 Siku iliyofuata mahakimu waliamuru Paulo na Sila wafunguliwe. Lakini Paulo akasema: “Walitupiga viboko hadharani bila kutuhukumu, ingawa sisi ni Waroma, na wakatutupa gerezani. Je, sasa wanatufukuza kwa siri? Hapana, haiwezekani! Acha waje watutoe nje wao wenyewe.” Baada ya kutambua kwamba wanaume hao wawili ni raia wa Roma, mahakimu hao “wakaogopa,” kwa sababu walikuwa wamekiuka haki zao.d Mambo yakageuka. Wanafunzi hao walipigwa viboko hadharani; sasa mahakimu walilazimika kuwaomba msamaha hadharani. Wakawasihi Paulo na Sila waondoke Filipi. Walikubali, lakini kwanza wakakitia moyo kikundi kipya cha wanafunzi kilichokuwa kikikua. Kisha wakaondoka.
-
-
“Vuka Uingie Makedonia”“Kutoa Ushahidi Kamili” Kuhusu Ufalme wa Mungu
-
-
d Kulingana na sheria ya Roma, raia alikuwa na haki ya kusikilizwa kabla ya kuhukumiwa naye hakupaswa kamwe kuadhibiwa hadharani kabla ya kuthibitishwa kuwa mwenye hatia.
-