Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • Kushinda Udhaifu wa Kibinadamu
    Mnara wa Mlinzi—2001 | Machi 15
    • 4. Paulo alitoa ushauri gani kwenye 1 Wakorintho 10:12, 13?

      4 Paulo alipowaandikia Wakristo walioishi Korintho—jiji lililojulikana kwa upotovu wake wa maadili—alitoa onyo la busara dhidi ya kishawishi na nguvu ya dhambi. Alisema: “Acheni yeye ambaye afikiri kuwa amesimama ajihadhari kwamba asianguke. Hakuna kishawishi ambacho kimewapata nyinyi ila kilicho kawaida kwa watu. Lakini Mungu ni mwaminifu, naye hatawaacha nyinyi mshawishwe kupita vile mwezavyo kuhimili, bali pamoja na hicho kishawishi ataifanya pia njia ya kutokea kusudi mweze kuvumilia hilo.” (1 Wakorintho 10:12, 13) Sisi sote—vijana kwa wazee, wanaume kwa wanawake—hukabili vishawishi vingi shuleni, kazini, au kwingineko. Kwa hiyo, acheni tuchunguze maneno ya Paulo na kuona yanamaanisha nini kwetu.

  • Kushinda Udhaifu wa Kibinadamu
    Mnara wa Mlinzi—2001 | Machi 15
    • 7. Kwa nini inafariji kujua kwamba wengine wamefaulu kukinza kishawishi?

      7 Tunapata faraja iliyoje kutokana na maneno ya Paulo: “Hakuna kishawishi ambacho kimewapata nyinyi ila kilicho kawaida kwa watu”! (1 Wakorintho 10:13) Mtume Petro aliandika: “Chukueni msimamo wenu dhidi ya [Ibilisi], mkiwa thabiti katika imani, mkijua kwamba mambo yaleyale kwa njia ya mateso yanatimizwa katika ushirika mzima wa ndugu zenu katika ulimwengu.” (1 Petro 5:9) Naam, wengine wamekabili vishawishi kama hivyo na kwa msaada wa Mungu wamefaulu kuvikinza, nasi pia twaweza kufanya hivyo. Hata hivyo, tukiwa Wakristo wa kweli tunaoishi katika ulimwengu uliopotoka, sote tunaweza kutarajia kushawishiwa siku moja. Basi, tunawezaje kuwa na hakika kwamba tutashinda udhaifu wa kibinadamu na kishawishi cha kufanya dhambi?

Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
Toka
Ingia
  • Kiswahili
  • Shiriki
  • Mapendezi
  • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
  • Masharti ya Utumiaji
  • Sera ya Faragha
  • Mpangilio wa Faragha
  • JW.ORG
  • Ingia
Shiriki