Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • Sababu kwa Nini Mlo wa Jioni wa Bwana Una Maana Kwako
    Mnara wa Mlinzi—1993 | Machi 15
    • Maneno haya ya mtume Paulo yaelewesha wazi zaidi juu ya ukumbusho wa kifo cha Kristo: “Nalipokea kwa Bwana niliyowapa nanyi, ya kuwa Bwana Yesu usiku ule aliotolewa alitwaa mkate, naye akiisha kushukuru akaumega, akasema, Huu ndio mwili wangu ulio kwa ajili yenu; fanyeni hivi kwa ukumbusho wangu. Na vivi hivi baada ya kula akakitwaa kikombe akasema, Kikombe hiki ni agano jipya katika damu yangu; fanyeni hivi kila mnywapo, kwa ukumbusho wangu. Maana kila mwulapo mkate huu na kukinywea kikombe hiki, mwaitangaza mauti ya Bwana hata ajapo.”—1 Wakorintho 11:23-26.

  • Sababu kwa Nini Mlo wa Jioni wa Bwana Una Maana Kwako
    Mnara wa Mlinzi—1993 | Machi 15
    • Kuuadhimisha Mara Nyingi Kadiri Gani?

      Ni nini maana ya maneno ya Paulo: “Kila [mara nyingi, NW] mwulapo mkate huu na kukinywea kikombe hiki, mwaitangaza mauti ya Bwana hata ajapo”? Wakristo wapakwa-mafuta waaminifu wangeshiriki mifano ya Ukumbusho “mara nyingi” mpaka wafe, baadaye wafufuliwe kwenye uhai wa kimbingu. Hivyo, mbele za Mungu na ulimwengu, wangetangaza mara nyingi imani yao katika uandalizi wa dhabihu ya Yesu. Kwa muda gani? “Hata ajapo,” akasema Paulo, kwa wazi akimaanisha kwamba miadhimisho hiyo ingeendelea mpaka kuwasili kwa Yesu ili kuwapokea wafuasi wake wapakwa-mafuta mbinguni kupitia ufufuo wakati wa “kuwapo” kwake. (1 Wathesalonike 4:14-17, NW) Hilo lapatana na maneno ya Kristo kwa wale mitume waaminifu-washikamanifu 11: “Nikienda na kuwaandalia mahali, nitakuja tena niwakaribishe kwangu; ili nilipo mimi, nanyi mwepo.”—Yohana 14:3.

      Je! kifo cha Kristo kikumbukwe kila siku au labda kila juma? Yesu alianzisha Mlo wa Jioni wa Bwana na akauawa katika Sikukuu ya Kupitwa, iliyokumbusha juu ya kukombolewa kwa Israeli kutoka katika utumwa wa Misri. Kwa kweli, yeye aitwa “Kristo kupitwa kwetu” kwa sababu yeye ndiye Mwana-Kondoo aliyetolewa dhabihu kwa ajili ya Wakristo. (1 Wakorintho 5:7, NW) Sikukuu ya Kupitwa iliadhimishwa mara moja tu kwa mwaka, katika Nisani 14. (Kutoka 12:6, 14; Mambo ya Walawi 23:5) Hilo ladokeza kwamba kifo cha Yesu chapasa kukumbukwa mara nyingi kadiri tu ambavyo Sikukuu ya Kupitwa ilikumbukwa—kila mwaka, si kila siku au juma.

      Kwa karne kadhaa wengi waliodai kuwa Wakristo walikumbuka kifo cha Yesu mara moja kwa mwaka. Kwa sababu walifanya hivyo katika Nisani 14, waliitwa Wakwotodesimi, linalomaanisha “wa kumi na nne.” Kuhusu wao, mwanahistoria J. L. von Mosheim aliandika hivi: “Wakristo wa Esia Ndogo walizoea kuadhimisha karamu hiyo takatifu, iliyokumbusha juu ya kuanzishwa kwa mlo wa jioni wa Bwana, na kifo cha Yesu Kristo, wakati uleule ambapo Wayahudi walikula mwana-kondoo wao wa Pasaka, yaani jioni ya siku ya kumi na nne ya mwezi wa kwanza [Nisani]. . . . Walihisi kuwa na wajibu wa kufuata mfano huo wa Yesu kama vile walivyofuata sheria.”

Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
Toka
Ingia
  • Kiswahili
  • Shiriki
  • Mapendezi
  • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
  • Masharti ya Utumiaji
  • Sera ya Faragha
  • Mpangilio wa Faragha
  • JW.ORG
  • Ingia
Shiriki