-
“Katika Hayo Lililo Kuu ni Upendo”Mnara wa Mlinzi—1990 | Novemba 15
-
-
“Katika Hayo Lililo Kuu ni Upendo”
“Basi, sasa inadumu imani, tumaini, upendo, haya matatu; na katika hayo lililo kuu ni upendo.”—1 WAKORINTHO 13:13.
1. Mstadi mmoja wa kuchunguza asili za binadamu alisema nini juu ya upendo?
MMOJA wa wastadi walio mashuhuri zaidi ulimwenguni katika uchunguzi wa asili za binadamu alisema hivi wakati mmoja: “Sisi twaelewa kwa mara ya kwanza katika historia ya jamii yetu [ya kibinadamu] kwamba ulio wa maana zaidi wa mahitaji yote ya msingi ya saikolojia ya kibinadamu ni uhitaji wa kupendwa. Huo uko katikati ya mahitaji yote ya kibinadamu kama vile jua letu lilivyo katikati ya mfumo-jua wetu likiwa linazungukwa na zile sayari. . . . Mtoto ambaye amekuwa hapendwi atofautiana sana na yule ambaye amekuwa akipendwa katika utendaji wa kemikali mwilini, tabia za utendaji wa chembe mwilini, na katika njia ya kufikiri. Huyo wa kwanza hata hukua kwa njia tofauti na huyu wa wa pili. Kile tujuacho sasa ni kwamba binadamu amezaliwa ili aishi kana kwamba maisha na upendo ni kitu kimoja. Bila shaka, hilo si jambo jipya. Hiyo yaonyesha uhalali wa yale Mahubiri juu ya Mlima.”
2. (a) Mtume Paulo alionyeshaje umaana wa upendo? (b) Ni maswali gani ambayo sasa yastahili ufikirio?
2 Ndiyo, kama alivyokubali mwanamume huyu mwenye elimu ya kilimwengu, ukweli huu juu ya umaana wa kuwa na upendo ili kuwe na hali njema ya kibinadamu si jambo jipya. Huenda ikawa ni sasa tu umekuja kuthaminiwa na watu wa ulimwengu wenye elimu, lakini ulitokea katika Neno la Mungu zaidi ya karne 19 zilizopita. Ndiyo sababu mtume Paulo angeweza kuandika hivi: “Basi, sasa inadumu imani, tumaini, upendo, haya matatu; na katika hayo lililo kuu ni upendo.” (1 Wakorintho 13:13) Je! wewe wajua kwa nini upendo ni mkubwa kuliko imani na tumaini? Kwa nini yaweza kusemwa kwamba ni upendo ulio mkuu kati ya sifa za Mungu na kati ya matunda ya roho yake?
-
-
“Katika Hayo Lililo Kuu ni Upendo”Mnara wa Mlinzi—1990 | Novemba 15
-
-
7. Upendo wa a·gaʹpe ni wa hali gani, na upendo huu umeonyeshwaje?
7 Ni neno gani la Kigiriki ambalo Paulo alitumia kwenye 1 Wakorintho 13:13, ambapo alitaja imani, tumaini, na upendo na kusema kwamba “katika hayo lililo kuu ni upendo”? Hapa neno ni a·gaʹpe, lile lile ambalo mtume Yohana alitumia aliposema: “Mungu ni upendo.” (1 Yohana 4:8, 16) Huu ni upendo wenye kuongozwa au kusimamiwa na kanuni. Huenda ukahusisha au usihusishe shauku na upenzi mwingi, lakini ni hisia-moyo isiyo na ubinafsi au hisia ambayo yahangaikia kufanyia wengine mema bila kujali mastahili ya mpokeaji wala manufaa zozote zenye kumjia mtoaji. Upendo wa aina hii ulisababisha Mungu atoe hazina yake iliyo kipenzi kikubwa zaidi cha moyo wake, Mwana wake mzaliwa wa pekee, Yesu Kristo, “ili kila mtu amwaminiye [anayejizoeza imani katika yeye, NW] asipotee, bali awe na uzima wa milele.” (Yohana 3:16) Kama vile Paulo atukumbushavyo vizuri sana: “Si rahisi mtu kufa kwa ajili ya mtu mwadilifu; labda mtu anaweza kuthubutu kufa kwa ajili ya mtu mwema. Lakini Mungu amethibitisha kwamba anatupenda, maana wakati tulipokuwa bado wenye dhambi, Kristo alikufa kwa ajili yetu.” (Warumi 5:7, 8, HNWW) Ndiyo, a·gaʹpe hufanyia wengine mema bila kujali cheo chao maishani au gharama kwa mwenye kuonyesha upendo huo.
Kwa Nini Ni Mkubwa Kuliko Imani na Tumaini?
8. Kwa nini a·gaʹpe ni mkubwa kuliko imani?
8 Lakini kwa nini Paulo alisema kwamba aina hii ya upendo (a·gaʹpe) ilikuwa kubwa kuliko imani? Aliandika hivi kwenye 1 Wakorintho 13:2: “Nijapokuwa na unabii, na kujua siri zote na maarifa yote, nijapokuwa na imani timilifu kiasi cha kuweza kuhamisha milima, kama sina upendo, si kitu mimi.” (Linganisha Mathayo 17:20.) Ndiyo, kama jitihada zetu za kupata maarifa na kukua katika imani zingefanywa kwa kusudi la ubinafsi, hiyo haingetuletea manufaa yoyote kutoka kwa Mungu. Vivyo hivyo, Yesu alionyesha kwamba watu fulani ‘wangefanya unabii kwa jina lake, na kwa jina lake watoe pepo, na kwa jina lake wafanye miujiza mingi’ lakini hawangepata kibali chake.—Mathayo 7:22, 23.
9. Kwa nini upendo ni mkubwa kuliko tumaini?
9 Kwa nini ile namna ya upendo wa a·gaʹpe ni kubwa pia kuliko tumaini? Kwa sababu huenda tumaini likawa lategemea mapendezi ya kibinafsi, mtu akihangaikia hasa manufaa atakazopata yeye mwenyewe, hali upendo “hautafuti mambo yake.” (1 Wakorintho 13:4, 5) Zaidi ya hilo, tumaini—kama lile la kuishi kupita “dhiki kubwa” kuingia katika ulimwengu mpya—hukoma wakati kile kitumainiwacho kipatwapo. (Mathayo 24:21) Kama asemavyo Paulo: “Kwa matumaini hayo [tumaini hili, NW] sisi tumekombolewa; lakini tumaini halina maana ikiwa tunakiona kile tunachotumainia. Maana ni nani anayetumaini kitu ambacho tayari anakiona? Kama tunakitumaini kile ambacho hatujakiona bado, basi, tunakingojea kwa uvumilivu.” (Warumi 8:24, 25, HNWW) Upendo wenyewe huvumilia mambo yote, nao haushindwi kamwe. (1 Wakorintho 13:7, 8) Hivyo, upendo usio na ubinafsi (a·gaʹpe) ni mkubwa kuliko ama imani ama tumaini.
-