Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • “Wafu Watafufuliwa”
    Mnara wa Mlinzi—1998 | Julai 1
    • 7. (a) Ni suala gani kuu ambalo Paulo alikazia? (b) Ni nani waliomwona Yesu aliyekuwa amefufuliwa?

      7 Katika mistari ya kwanza miwili ya 1 Wakorintho sura ya 15, Paulo ataja kichwa cha mazungumzo yake: “Nawajulisha nyinyi, akina ndugu, habari njema niliyowatangazia, mliyoipokea pia, ambayo katika hiyo mwasimama pia, ambayo kupitia hiyo nyinyi pia mnaokolewa, . . . isipokuwa, kwa kweli, mwe mlipata kuwa waamini bila kusudi lolote.” Wakorintho walikuwa wameipokea kweli bure, ikiwa walishindwa kusimama imara katika habari njema. Paulo aliendelea kusema hivi: “Niliwapa nyinyi, miongoni mwa mambo ya kwanza, lile nililolipokea pia, kwamba Kristo alikufa kwa ajili ya dhambi zetu kulingana na Maandiko; na kwamba alizikwa, ndiyo, kwamba amefufuliwa siku ya tatu kulingana na Maandiko; na kwamba alionekana kwa Kefa, kisha kwa wale kumi na wawili. Baada ya hilo alionekana kwa zaidi ya ndugu mia tano kwa wakati mmoja, ambao walio wengi kati yao wabaki hadi wakati wa sasa, lakini baadhi yao wamelala usingizi katika kifo. Baada ya hilo alionekana kwa Yakobo, kisha kwa mitume wote; lakini mwisho wa wote alionekana pia kwangu kama kwamba kwa mmoja aliyezaliwa kabla ya wakati wake.”—1 Wakorintho 15:3-8.

  • “Wafu Watafufuliwa”
    Mnara wa Mlinzi—1998 | Julai 1
    • 9 Kristo pia alionekana kwa kikundi kikubwa zaidi, “ndugu zaidi ya mia tano.” Kwa kuwa ni katika Galilaya tu alikokuwa na idadi kubwa hivyo ya wafuasi, huenda huo ukawa ni ule wakati ambao umeelezwa kwenye Mathayo 28:16-20, Yesu alipotoa amri ya kufanya wanafunzi. Hao watu wangeweza kutoa ushuhuda wenye nguvu kama nini! Baadhi yao walikuwa bado hai mwaka wa 55 W.K. wakati Paulo alipotunga barua yake ya kwanza kwa Wakorintho. Ingawa hivyo, ona kwamba wale waliokuwa wamekufa walitajwa kuwa “wamelala usingizi katika kifo.” Walikuwa bado hawajafufuliwa ili kupokea thawabu yao ya kimbingu.

Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
Toka
Ingia
  • Kiswahili
  • Shiriki
  • Mapendezi
  • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
  • Masharti ya Utumiaji
  • Sera ya Faragha
  • Mpangilio wa Faragha
  • JW.ORG
  • Ingia
Shiriki