-
Jifunze Kutoka kwa Ndugu Mdogo wa YesuMnara wa Mlinzi (Funzo)—2022 | Januari
-
-
ENDELEA KUWA MNYENYEKEVU KAMA YAKOBO
Yakobo alijinyenyekeza Yesu alipomtokea, na tangu wakati huo akawa mwanafunzi mwaminifu wa Kristo (Tazama fungu la 5 hadi 7)
5. Yakobo aliitikiaje Yesu alipomtokea baada ya kufufuliwa?
5 Yakobo alianza kuwa mfuasi mshikamanifu wa Yesu lini? Baada ya Yesu kufufuliwa, “alimtokea Yakobo, kisha mitume wote.” (1 Kor. 15:7) Baada ya kukutana na Yesu, Yakobo akawa mwanafunzi wake. Alikuwepo mitume walipokuwa wakisubiri roho takatifu iliyoahidiwa, katika chumba cha juu huko Yerusalemu. (Mdo. 1:13, 14) Baadaye, Yakobo alikuwa na pendeleo la kutumikia akiwa mshiriki wa baraza linaloongoza la karne ya kwanza. (Mdo. 15:6, 13-22; Gal. 2:9) Na muda fulani kabla ya mwaka wa 62 W.K., aliongozwa na roho kuwaandikia barua Wakristo watiwa-mafuta. Barua hiyo inatunufaisha sisi leo, iwe tuna tumaini la kuishi mbinguni au duniani. (Yak. 1:1) Kulingana na mwanahistoria wa karne ya kwanza, Yosefo, Yakobo aliuawa kufuatia agizo la Kuhani Mkuu Myahudi Anania Mdogo. Yakobo aliendelea kuwa mwaminifu kwa Yehova hadi mwisho wa maisha yake hapa duniani.
-