-
Historia ya Waroma Inatufunza Somo FulaniMnara wa Mlinzi—2002 | Juni 15
-
-
Historia ya Waroma Inatufunza Somo Fulani
“IKIWA, kama wanadamu, nimepigana na mahayawani-mwitu katika Efeso.” Watu fulani hufikiri kwamba maneno hayo, yanayopatikana katika andiko la 1 Wakorintho 15:32, yanamaanisha kwamba mtume Paulo alihukumiwa kupigana katika uwanja fulani wa Waroma. Iwe Paulo alipigana au la, siku hizo lilikuwa jambo la kawaida watu kupigana viwanjani hadi kufa. Historia inasema nini kuhusu viwanja hivyo na mambo yaliyofanyika huko?
-
-
Historia ya Waroma Inatufunza Somo FulaniMnara wa Mlinzi—2002 | Juni 15
-
-
Huenda ukajiuliza, ‘Wapiganaji hao walikuwa nani?’ Huenda walikuwa watumwa, wahalifu waliohukumiwa kifo, wafungwa wa kivita, au watu waliochochewa na tamaa ya makuu au utajiri. Wote walizoezwa katika shule zilizokuwa kama jela. Kitabu Giochi e spettacoli (Michezo na Tamasha) kinaripoti kwamba wakati wa mazoezi wapiganaji walisimamiwa daima na walinzi na walipewa nidhamu kali sana. Walitazamiwa kutii sheria ngumu sana na wangeweza kuadhibiwa vikali sana . . . Kwa sababu ya kutendwa hivyo, mara nyingi watu fulani walijiua au wakaasi.” Shule kubwa zaidi ya kuzoeza wapiganaji huko Roma ilikuwa na vyumba vidogo vya watu wapatao elfu moja. Kila mtu alizoezwa ustadi fulani wa kupigana. Wengine walipigana kwa kutumia bamba, ngao, na upanga, nao wengine walitumia nyavu na mkuki wenye ncha tatu. Wengine walizoezwa kupigana na wanyama katika onyesho la uwindaji lililopendwa sana. Je, Paulo alikuwa akizungumza kuhusu pigano hilo?
-
-
Historia ya Waroma Inatufunza Somo FulaniMnara wa Mlinzi—2002 | Juni 15
-
-
Onyesho la uwindaji lilifanywa asubuhi. Wanyama wa mwitu wa kila aina waliingizwa kwa nguvu uwanjani. Wahudhuriaji walifurahia sana pigano kati ya fahali na dubu. Mara nyingi wanyama hao walifungwa pamoja ili wapigane hadi mmoja afe, kisha mnyama aliyebaki aliuawa na mwindaji. Mashindano mengine yaliyopendwa sana yalihusisha simba na simbamarara, au tembo na dubu. Wawindaji walidhihirisha ustadi wao wa kuua wanyama ambao waliletwa kutoka sehemu zote za milki hiyo bila kujali gharama iliyohusika. Wanyama hao walitia ndani chui, vifaru, viboko, twiga, fisi, ngamia, mbwa-mwitu, nguruwe-mwitu, na paa.
Mandhari kwenye viwanja hivyo yalifanya watu wasisahau maonyesho hayo ya uwindaji. Miamba, vidimbwi, na miti ilitumiwa ili mahali hapo pafanane na misitu. Katika viwanja fulani, wanyama walitokea tu kana kwamba kwa mizungu, wakipandishwa na lifti za chini ya ardhi na kutokea milango ya sakafuni. Jambo lililowavutia sana watu katika onyesho la uwindaji ni tabia zisizo za kawaida za wanyama hao. Hata hivyo walivutiwa zaidi na ukatili.
-