-
Wanawake Wakristo—Kudumisha Ukamilifu Mahali pa KaziMnara wa Mlinzi—1987 | Machi 15
-
-
Mwanamke mmoja mwenye utambuzi jina lake Betty anachukua hatua nyingine ya tahadhari. Yeye anasema: “Mimi ninakuwa mwangalifu sana juu ya kushirikiana na wafanya kazi wenzangu kwa sababu adili zao haziko sawa na zangu.” (1 Wakorintho 15:33) Hiyo haimaanishi mtu ajitenge mbali au kuwa mwenye uhasama kwa wafanya kazi wenzake. Lakini wakati wao wanaposisitizia kuzungumzia mambo yenye kuudhi Mkristo, usisitesite kujiondoa kati yao. (Waefeso 5:3, 4) Kule kusikiliza tu maongezi kama hayo ya ukosefu wa adili kungeweza kuwapa wanaume kazini wazo la kwamba wewe ungeitikia matongozi yao.
-
-
Wanawake Wakristo—Kudumisha Ukamilifu Mahali pa KaziMnara wa Mlinzi—1987 | Machi 15
-
-
Hatimaye, mwanamke mwenye utambuzi anaepuka hali za kuachisha msimamo. Mwaliko wa kunywa kileo au kubaki kazini baada ya saa za kazi kwa sababu isiyo wazi huenda hata ukawa ni mtego! (Linganisha 2 Samweli 13:1-14.) “Mwenye busara huyaona mabaya na kujificha,” inasema mithali yenye hekima.—Mithali 22:3.
-