-
Tito—“Mfanyakazi Mwenzi kwa Ajili ya Masilahi Yenu”Mnara wa Mlinzi—1998 | Novemba 15
-
-
Barua ya Paulo kwa Wakorintho yafunua kwamba kwanza aliwaandikia ‘wakome kuchangamana katika ushirika na waasherati.’ Alilazimika kuwaambia wamwondoe mwasherati asiyetubu miongoni mwao. Naam, Paulo aliwaandikia barua kali, akifanya hivyo “kwa machozi mengi.” (1 Wakorintho 5:9-13; 2 Wakorintho 2:4) Wakati uleule, Tito alikuwa ametumwa Korintho ili kusaidia kuchanga ambako kulikuwa kukiendelea huko kwa ajili ya Wakristo wa Yudea wenye uhitaji. Labda, pia alitumwa kuchunguza jinsi Wakorintho walivyoitikia barua ya Paulo.—2 Wakorintho 8:1-6.
-
-
Tito—“Mfanyakazi Mwenzi kwa Ajili ya Masilahi Yenu”Mnara wa Mlinzi—1998 | Novemba 15
-
-
Vipi ile sehemu nyingine ya kazi ya Tito huko Korintho—kusimamia mchango kwa ajili ya watakatifu katika Yudea? Tito alikuwa akishughulikia hilo vilevile, kama vile habari ipatikanayo katika 2 Wakorintho ionyeshavyo. Labda barua hiyo iliandikwa Makedonia mwishoni mwa mwaka wa 55 W.K., upesi baada ya Tito kukutana na Paulo. Paulo aliandika kwamba Tito ambaye alikuwa ameanzisha mchango, sasa alikuwa akitumwa arudi akiwa na wasaidizi wawili wasiotajwa majina ili kuukamilisha. Akipendezwa na Wakorintho sana, Tito alikuwa tayari kurudi. Alipokuwa akirudi Korintho, yaelekea Tito alikuwa akibeba barua ya pili iliyopuliziwa ambayo Paulo aliwaandikia Wakorintho.—2 Wakorintho 8:6, 17, 18, 22.
-