-
Je, Wajua?Mnara wa Mlinzi—2010 | Agosti 1
-
-
Mtume Paulo alimaanisha nini kwa maneno “maandamano yenye shangwe”?
▪ Paulo aliandika hivi: “Mungu . . . hutuongoza katika maandamano yenye shangwe ya ushindi kwa kushirikiana na Kristo naye huifanya harufu ya ujuzi juu yake yeye ifahamike kupitia sisi kila mahali! Kwa maana kwa Mungu sisi ni harufu tamu ya Kristo katikati ya wale wanaookolewa na katikati ya wale wanaoangamia; kwa hawa wa mwisho ni harufu inayotoka katika kifo mpaka kifo, kwa wale wa kwanza ni harufu inayotoka katika uzima mpaka uzima.”—2 Wakorintho 2:14-16.
Paulo alikuwa akirejelea zoea la Waroma la kumfanyia sherehe za maandamano jemadari ambaye alikuwa amewashinda maadui wa Taifa. Katika sherehe za maandamano kama hizo, kulikuwa na maonyesho ya hadharani ya wafungwa wa vita pamoja na nyara zilizokusanywa vitani na ng’ombe-dume ambao wangetolewa kama dhabihu huku jemadari aliyepata ushindi pamoja na jeshi lake wakisifiwa na raia. Maandamano hayo yalipoisha, ng’ombe-dume hao walichinjwa na huenda wengi wa wafungwa hao waliuawa.
Kitabu kimoja cha marejeo (The International Standard Bible Encyclopedia) kinasema kuwa maneno “harufu tamu ya Kristo” yanayotumiwa kuonyesha kuwa watu fulani wangekufa na wengine kuendelea kuishi, ‘huenda yanatokana na zoea la Waroma la kuvukiza uvumba wakati wa maandamano hayo. Harufu ya uvumba ambayo iliwakilisha ushindi kwa jemadari na jeshi lake, iliwakumbusha wale wafungwa, kuhusu kifo ambacho huenda kingewapata.’a
-
-
Je, Wajua?Mnara wa Mlinzi—2010 | Agosti 1
-
-
a Kwa maelezo kuhusu maana ya kiroho ya mfano huo wa Paulo, ona Mnara wa Mlinzi, Novemba 15, 1990 (15/11/1990), ukurasa 27.
[Picha katika ukurasa wa 23]
Sehemu ya mchoro ukionyesha maandamano yenye shangwe ya Waroma katika karne ya pili W.K.
[Hisani]
Photograph taken by courtesy of the British Museum
-