-
“Kujawa na Shangwe na Roho Takatifu”“Kutoa Ushahidi Kamili” Kuhusu Ufalme wa Mungu
-
-
10. Eleza jinsi safari ya kutoka Perga kuelekea Antiokia ya Pisidia ilivyokuwa.
10 Walipofika Perga, Yohana Marko aliwaacha Paulo na Barnaba, akarudi Yerusalemu. Haieleweki kwa nini aliondoka. Paulo na Barnaba waliendelea na safari kutoka Perga hadi Antiokia ya Pisidia, jiji lililokuwa katika wilaya ya Galatia. Safari hiyo haikuwa rahisi, kwa kuwa Antiokia ya Pisidia iko mita 1,100 juu ya usawa wa bahari. Mara nyingi njia za milimani zilikuwa na wanyang’anyi. Isitoshe, huenda Paulo alikuwa na matatizo ya afya pia.h
-