Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • Silaha, Mavazi ya Silaha
    Ufahamu wa Kina wa Maandiko
    • Neno la Kigiriki beʹlos (kombora) linatokana na mzizi balʹlo, unaomaanisha “tupa.” Mtume Paulo alitumia neno hilo la Kigiriki alipoandika kuhusu “makombora” ambayo mtu anaweza kuyazima kwa kutumia ngao kubwa ya imani. (Efe 6:16, maelezo ya chini) Kwa Waroma, vishale vilitengenezwa kwa matete, na kwenye sehemu ya chini, chini ya ncha, kulikuwa na chombo cha chuma ambacho kingeweza kujazwa mafuta mepesi yanayowaka. Hivyo, kishale kilirushwa kwa upinde uliolegea, kwa kuwa kukirusha kwa kutumia upinde uliokazwa kungetokeza moto. Kujaribu kuzima kombora kama hilo kwa maji kungeongeza tu moto, na njia pekee ya kulizima ilikuwa ni kwa kulifunika na udongo.

  • Silaha, Mavazi ya Silaha
    Ufahamu wa Kina wa Maandiko
    • “Ngao kubwa” (Kiebr., tsin·nahʹ) zilibebwa na wanajeshi wenye nguvu waliojihami kwa silaha (2Nya 14:8) na wakati mwingine na mbeba silaha. (1Sa 17:7, 41) Zilikuwa ama za duara au za mstatili kama mlango. Kwa kufaa, “ngao kubwa” sawa na hizo zimetajwa katika Waefeso 6:16 kwa kutumia neno la Kigiriki thy·re·osʹ (linalotokana na thyʹra, linalomaanisha “mlango”). Tsin·nahʹ ilikuwa na ukubwa unaoweza kufunika mwili wote. (Zb 5:12) Pindi fulani ilitumiwa kutengeneza mistari ya mbele ya vita iliyo imara huku fumo zikizochomoza. Pindi fulani ngao kubwa inatajwa pamoja na fumo na mkuki kama njia ya kurejelea silaha za vita kwa ujumla.​—1Nya 12:8, 34; 2Nya 11:12.

  • Silaha, Mavazi ya Silaha
    Ufahamu wa Kina wa Maandiko
    • Sehemu yenye kutokeza ya mavazi ya silaha ya kiroho ni “ngao kubwa ya imani.” Kama ngao kubwa inayofunika karibu mwili wote, imani katika Yehova Mungu na katika uwezo wake wa kutimiza ahadi zake itamsaidia Mkristo “[kuizima] mishale yote inayowaka moto ya yule mwovu.” (Efe 6:16; linganisha Zb 91:4.) Imani itamsaidia Mkristo kushinda mashambulizi ya roho waovu, kupinga vishawishi vya ukosefu wa maadili, kuepuka kutamani vitu vya kimwili, na kutoshindwa na woga, shaka, au huzuni iliyopita kiasi.​—Mwa 39:7-12; Ebr 11:15; 13:6; Yak 1:6; 1Th 4:13.

Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
Toka
Ingia
  • Kiswahili
  • Shiriki
  • Mapendezi
  • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
  • Masharti ya Utumiaji
  • Sera ya Faragha
  • Mpangilio wa Faragha
  • JW.ORG
  • Ingia
Shiriki