-
Songa Mbele Kuuelekea Mradi!Mnara wa Mlinzi—1990 | Novemba 15
-
-
Endeleeni Kusonga Mbele Kuuelekea Mradi
Ndipo mtume awaonyesha Wafilipi mahali pa kuweka uhakika wao wasongapo mbele kuuelekea mradi. (3:1-21) Wapasa kuwekwa katika Yesu Kristo, si katika mnofu wala katika tohara kama watu fulani walivyokuwa wakifanya. Paulo alifikiria sifa za ustahili wake wa kimnofu kuwa takataka kwa sababu ya “uzuri [thamani, NW] usio na kiasi wa kumjua Kristo.” Mtume alikuwa ‘akikaza mwendo, aifikilie mede ya thawabu ya mwito mkuu wa Mungu katika Kristo Yesu’ na akawatia moyo Wafilipi wawe na mtazamo ule ule wa akilini.
-
-
Songa Mbele Kuuelekea Mradi!Mnara wa Mlinzi—1990 | Novemba 15
-
-
[Sanduku/Picha katika ukurasa wa 25]
Kuuelekea Mradi: “Nikiyasahau yaliyo nyuma, nikiyachuchumilia yaliyo mbele,” akaandika Paulo, “nakaza mwendo, niifikilie mede ya thawabu ya mwito mkuu wa Mungu katika Kristo Yesu.” (Wafilipi 3:13, 14) Mtume alikuwa akijitahidi sana kama mtu aliye katika mbio. Hakupoteza wakati na jitihada akitazama nyuma bali alisonga mbele kuelekea mradi wake—kama mkimbiaji mwenye kujikaza avuke mstari wa kumalizia. Kwa Paulo na Wakristo wengine wapakwa-mafuta, zawadi ilikuwa uhai wa kimbingu kwa kufufuliwa baada ya kumaliza mwendo wa kidunia wa uaminifu kwa Mungu. Matumaini yetu yawe ni ya kimbingu au ya kidunia, acheni tushike uaminifu wa kimaadili kwa Yehova na tusonge mbele kuuelekea mradi tukiwa Mashahidi wake.—2 Timotheo 4:7.
-