-
Kutambulisha “Mtu wa Kuasi [Sheria]”Mnara wa Mlinzi—1990 | Februari 1
-
-
6. Ni habari gani zaidi ambazo Paulo atoa kuhusu mwasi sheria huyo?
6 Paulo aeleza zaidi juu ya mtu huyu mwenye kuasi sheria, akisema: “Yeye amejiweka katika hali ya kupinga na hujiinua mwenyewe juu ya kila mmoja aitwaye ‘mungu’ au kitu cha uchaji, hivi kwamba yeye huketi katika hekalu la Yule Mungu, akijionyesha peupe kuwa ni mungu.” (2 Wathesalonike 2:4, NW) Kwa hiyo Paulo aonya kwamba Shetani angeinua mwasi sheria, kitu bandia cha uchaji, ambaye hata angejiweka mwenyewe juu ya sheria ya Mungu.
-
-
Kutambulisha “Mtu wa Kuasi [Sheria]”Mnara wa Mlinzi—1990 | Februari 1
-
-
Kujikweza Wenyewe
10. Yule mwasi sheria amekuwa na uhusiano gani pamoja na watawala wa kisiasa?
10 Historia yaonyesha kwamba wale walio katika jamii hii ya mtu wa kuasi wameonyesha kiburi na majivuno mengi sana hivi kwamba kwa kweli wameamrisha watawala wa ulimwengu. Kwa kusingizia kufuata fundisho la ‘haki ya kimungu ya wafalme,’ makasisi wamedai kwamba wao ndio wapatanishi muhimu kati ya watawala na Mungu. Wamewavika taji wafalme na wamaliki na kuwaondoa katika kiti cha kifalme na wakaweza kugeuza matungamo ya watu yaunge mkono au yawe dhidi ya watawala. Kwa kweli, wao wamesema, kama walivyosema wakuu wa makuhani Wayahudi ambao walimkataa Yesu: “Sisi hatuna mfalme ila Kaisari.” (Yohana 19:15) Hata hivyo, Yesu alifundisha wazi hivi: “Ufalme wangu si sehemu ya ulimwengu huu.”—Yohana 18:36, NW.
11. Makasisi wamejikwezaje?
11 Ili ijikweze hata zaidi juu ya watu wa kawaida, jamii hii yenye kuasi sheria imejichagulia mavazi tofauti, kwa kawaida yakiwa meusi. Zaidi ya hilo, wamejivika aina zote za mapambo yenye uvutio wa kifalme, pamoja na mataji, misalaba, na kofia za kiaskofu. (Linganisha Mathayo 23:5, 6.) Lakini Yesu na wafuasi wake hawakuwa na nguo za jinsi hiyo; walivalia kama watu wa kawaida. Pia makasisi wamejitwalia vyeo kama “Baba,” “Baba Mtakatifu,” “Reverendi,” “Reverendi Mkubwa Zaidi,” “Mtukufu,” na “Mwadhamu,” ambavyo vyaongezea ‘kujiinua wenyewe juu ya kila mtu.’ Hata hivyo, Yesu alifundisha hivi kuhusu vyeo vya kidini: “Msimwite mtu baba duniani.” (Mathayo 23:9) Vivyo hivyo, Elihu, katika kuwakanusha wafariji wanafiki wa Ayubu, alisema: “Tafadhali, nisiupendelee uso wa mtu; wala sitajipendekeza kwa mtu ye yote.”—Ayubu 32:21.
-