-
Kutambulisha “Mtu wa Kuasi [Sheria]”Mnara wa Mlinzi—1990 | Februari 1
-
-
Mwanzo wa Mtu wa Kuasi Sheria
4. Ni nani mwanzishi na mtegemezaji wa yule mtu wa kuasi sheria?
4 Ni nani aliyeanzisha na kuunga mkono mtu huyu wa kuasi sheria? Paulo ajibu hivi: “Kuwapo kwa huyo mwenye kuasi sheria ni kulingana na uendeshaji shughuli wa Shetani pamoja na kila kazi yenye nguvu nyingi na ishara na vionyeshi vyenye kusema uwongo na pamoja na kila udanganyifu usio mwadilifu kwa ajili ya wale wanaoangamia, liwe kama lipizo kwa sababu wao hawakuukubali upendo wa ule ukweli ili wapate kuokolewa.” (2 Wathesalonike 2:9, 10, NW) Kwa hiyo Shetani ndiye baba na mtegemezaji wa mtu wa kuasi sheria. Na sawa na vile Shetani apinga Yehova, makusudi Yake, na watu Wake, ndivyo pia afanyavyo mtu wa kuasi sheria, awe atambua au hatambui hivyo.
5. Ni msiba gani wamngoja mwasi sheria huyo na wale wenye kumfuata?
5 Wale ambao waambatana na mtu huyu wa kuasi sheria watapata msiba ule ule utakaompata yeye—uharibifu: “Hapo ndipo atakapofunuliwa yule asi, ambaye Bwana Yesu atamwua kwa pumzi ya kinywa chake, na kumwangamiza kwa ufunuo wa kuwapo kwake.” (2 Wathesalonike 2:8) Wakati huo wa kuharibiwa kwa mtu wa kuasi sheria na kwa wenye kumuunga mkono (“hao wanaopotea”) utakuja karibuni “wakati wa kufunuliwa kwake Bwana Yesu kutoka mbinguni pamoja na malaika wa uweza wake; katika mwali wa moto; huku akiwalipiza kisasi wao wasiomjua Mungu, na wao wasioitii Injili ya Bwana wetu Yesu; watakaoadhibiwa kwa maangamizi ya milele.”—2 Wathesalonike 1:6-9.
-
-
Kutambulisha “Mtu wa Kuasi [Sheria]”Mnara wa Mlinzi—1990 | Februari 1
-
-
Kutambulisha Mwasi Sheria Huyo
7. Kwa nini twakata shauri kwamba Paulo hakuwa akiongea kuhusu mtu mmoja, na mtu wa kuasi sheria asimamia nini?
7 Je! Paulo alikuwa akinena juu ya mtu mmoja? Hapana, kwa maana yeye ataarifu kwamba “mtu” huyu alikuwa akionekana wazi katika siku ya Paulo na angeendelea kuwako mpaka Yehova amharibu kwenye mwisho wa mfumo huu. Hivyo, yeye amekuwako kwa karne nyingi. Kwa uwazi, hakuna mtu halisi ambaye ameishi muda mrefu jinsi hiyo. Kwa hiyo ni lazima usemi “mtu wa kuasi [sheria]” uwe wasimamia baraza la watu, au jamii.
8. Mtu wa kuasi sheria ni nani, na ni nini baadhi ya mambo yenye kumtambulisha?
8 Wao ni akina nani? Ushuhuda waonyesha kwamba wao ni lile baraza la makasisi wenye kiburi, wenye kujitakia makuu wa Jumuiya ya Wakristo, ambao kwa muda wa karne zilizopita wamejipandisha juu katika mamlaka ya kuwa wakijiamulia mambo kama watakavyo. Hilo laweza kuonwa kwa uhakika wa kwamba kuna maelfu ya dini tofauti-tofauti na mafarakano ya ibada katika Jumuiya ya Wakristo, kila moja ikiwa na makasisi wayo yenyewe, na bado kila moja ikihitilafiana na nyinginezo katika jambo fulani la fundisho au zoea. Hali hii ya kugawanyika ni ushuhuda wa wazi kwamba hazifuati sheria ya Mungu. Haziwezi kuwa zatoka kwa Mungu. (Linganisha Mika 2:12; Marko 3:24; Warumi 16:17; 1 Wakorintho 1:10.) Jambo la ujumla lililo katika dini zote hizi ni kwamba haziyashiki imara mafundisho ya Biblia, kwa kuwa zimekwisha kuvunja ile kanuni ya kwamba: ‘Msiyapite yale yaliyoandikwa.’—1 Wakorintho 4:6; ona pia Mathayo 15:3, 9, 14.
9. Ni imani gani zisizo za Kimaandiko ambazo yule mwasi sheria ameweka mahali pa kweli za Biblia?
9 Hivyo, mwasi sheria huyu ni jumla ya watu wengi: makasisi wa Jumuiya ya Wakristo. Wote pamoja, wawe ni mapapa, mapadri, mapatriaki, au wahubiri wa Kiprotestanti, hushiriki daraka kwa dhambi za kidini za Jumuiya ya Wakristo. Wamebadili kweli za Mungu kwa uwongo wa kipagani, wakifundisha mafundisho yasiyo ya Kimaandiko kama vile kutokufa kwa nafsi ya kibinadamu, moto wa helo, pargatori, na Utatu. Wao ni kama viongozi wa kidini ambao Yesu aliambia hivi: “Ninyi ni wa baba yenu, Ibilisi, na tamaa za baba yenu ndizo mpendazo kuzitenda. . . . Yeye ni mwongo, na baba wa huo [uwongo].” (Yohana 8:44) Mazoea yao yawafichua pia kuwa waasi sheria, kwa maana wao hushiriki katika utendaji mbalimbali wenye kuvunja sheria za Mungu. Kwa watu hao Yesu asema hivi: “Ondokeni kwangu, ninyi mtendao maovu.”—Mathayo 7:21-23.
-