-
Kuna Ubaya Gani Kuchuma Pesa?Amkeni!—1997 | Septemba 22
-
-
Biblia hushughulika na maswali aya haya. Mtume Paulo aliandika: “Wale waazimiao kuwa matajiri huanguka ndani ya kishawishi na mtego na tamaa nyingi zisizo za akili na zenye kuumiza, ambazo hutumbukiza watu ndani ya uharibifu na uangamizo. Kwa maana kupenda fedha ni mzizi wa mambo mabaya ya namna zote, na kwa kujitahidi kufikilia kupenda huku wengine wameongozwa wapotee njia kutoka kwenye imani na wamejichoma wenyewe kotekote kwa maumivu mengi.”—1 Timotheo 6:9, 10.
-
-
Kuna Ubaya Gani Kuchuma Pesa?Amkeni!—1997 | Septemba 22
-
-
Kwa usahihi, basi, Paulo asema kuwa “kupenda fedha [kunakochukua wakati mwingi mno] ni mzizi wa mambo mabaya ya namna zote.” Likiwa tokeo, wengi “wameongozwa wapotee njia kutoka kwenye imani na wamejichoma kotekote kwa maumivu mengi.” Chukua kwa kielelezo, kijana tutakayemwita Rory. Kufikia umri wa miaka 12 alianza kucheza kamari. “Ilikuwa njia ya kupata pesa bila kufanya chochote,” akumbuka. Punde si punde, alikuwa na deni la mamia ya dola na akiwapuuza marafiki, familia na kazi ya shule. “Nilijaribu kuacha,” akiri, lakini alishindwa mara nyingi. Aliendelea ‘kujichoma mwenyewe kotekote kwa maumivu mengi’ hadi alipotafuta msaada akiwa na umri wa miaka 19. Mwandikaji Douglas Kennedy hatii chumvi wakati ambapo, katika kitabu chake Chasing Mammon, anaita ufuatiaji wa pesa “ono lenye kuvuruga.”
-