Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • Dhambi
    Ufahamu wa Kina wa Maandiko
    • Kama masimulizi hayo yanavyofunua, tamaa isiyofaa ilianza kufanya kazi ndani ya mwanamke huyo. Badala ya kuitikia kwa njia ya kuchukizwa kabisa na kuwa na ghadhabu ya uadilifu aliposikia uadilifu wa sheria ya Mungu ukitiliwa shaka, sasa alianza kuutazama ule mti kuwa wenye kutamanika. Alitamani kitu ambacho kwa haki kilikuwa ni cha Yehova Mungu akiwa Mwenye Enzi Kuu wake—uweza na haki yake ya kuamua ni nini kilicho chema na kilicho kibaya kwa ajili ya viumbe vyake. Kwa hiyo, sasa yeye alikuwa ameanza kujipatanisha na njia, viwango, na mapenzi ya mpinzani huyo, aliyekuwa amepinga Muumba wake na vilevile kichwa chake aliyewekwa rasmi, mumeye. (1Ko 11:3) Kwa kutia tumaini lake katika maneno ya Mshawishi huyo, yeye alijiruhusu ashawishwe, akala tunda, na kwa njia hiyo akaifunua dhambi iliyokuwa imezaliwa katika moyo na akili yake.—Mwa 3:6; 2Ko 11:3; linganisha Yak 1:14, 15; Mt 5:27, 28.

  • Dhambi
    Ufahamu wa Kina wa Maandiko
    • Katika Maandiko ya Kiebrania kuna marejezo kama hayo juu ya dhambi kutendwa na watu ambao ‘walihalifu,’ au ‘kuvunja’ (Kiebr.,ʽa·var′) agano la Mungu au maagizo hususa.—Hes 14:41; Kum 17:2, 3; Yos 7:11, 15; 1Sa 15:24, UV; Isa 24:5; Yer 34:18.

  • Enzi Kuu
    Ufahamu wa Kina wa Maandiko
    • Alipokabili uasi katika nyumba yake, Adamu ambaye pia hakumthamini wala kumpenda Muumba na Mwandalizi wake, hakuwa mshikamanifu kwa Mungu wake alipojaribiwa, basi akakubali kushawishiwa na Hawa. Adamu alipoteza imani katika Mungu na uwezo wa Mungu wa kumwandalia mtumishi wake mshikamanifu vitu vyote vizuri. (Linganisha na jambo ambalo Yehova alimwambia Daudi baada ya kufanya dhambi na Bath-sheba, katika 2Sa 12:7-9.) Jibu la Adamu alipoulizwa kuhusu kosa lake linaonyesha kwamba alimkasirikia Yehova: “Mwanamke uliyenipa nikae naye, alinipa tunda kutoka katika mti huo, basi nikala.” (Mwa 3:12) Hakuamini uwongo wa Nyoka kwamba hangekufa, kama Hawa alivyoamini, lakini wote wawili, Adamu na Hawa, waliazimia kujitegemea na kumwasi Mungu kimakusudi.​—1Ti 2:14.

Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
Toka
Ingia
  • Kiswahili
  • Shiriki
  • Mapendezi
  • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
  • Masharti ya Utumiaji
  • Sera ya Faragha
  • Mpangilio wa Faragha
  • JW.ORG
  • Ingia
Shiriki