Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • Waangalizi Wanaochunga Kundi
    Tengenezo Linalofanya Mapenzi ya Yehova
    • 11 Wanaume wanaostahili kuwa waangalizi wanaonyesha kiasi katika mazoea na wanaposhughulika na wengine. Hawapaswi kuwa washupavu. Badala yake, wanapaswa kuwa na usawaziko na wanaojidhibiti. Wanapaswa kuwa na kiasi katika kula, kunywa, tafrija, mambo wanayopenda, na burudani. Wanakunywa pombe kwa kiasi ili wasishtakiwe kwa madai ya ulevi au wasiwe na shtaka la kuwa walevi. Mtu ambaye hisi zake zimepumbazwa na pombe hushindwa kujidhibiti, naye hawezi kushughulikia mahitaji ya kiroho ya kutaniko.

  • Waangalizi Wanaochunga Kundi
    Tengenezo Linalofanya Mapenzi ya Yehova
    • 14 Pia, yule anayestahili kutumikia akiwa mwangalizi kutanikoni anapaswa kuwa mwenye utimamu wa akili. Hilo linamaanisha awe mtulivu, na asiyefanya uamuzi haraka-haraka. Anazijua vizuri kanuni za Yehova na jinsi zinavyotumika. Mtu mwenye utimamu wa akili yuko tayari kukubali ushauri na mwongozo. Yeye si mnafiki.

  • Waangalizi Wanaochunga Kundi
    Tengenezo Linalofanya Mapenzi ya Yehova
    • 15 Paulo alimkumbusha Tito kwamba mwangalizi ni mtu anayependa mema. Anapaswa kuwa mwadilifu na mshikamanifu. Sifa hizo zitaonekana anaposhughulika na wengine na anapotetea kwa uthabiti yale yaliyo sawa na yaliyo mema. Hayumbi-yumbi katika ujitoaji wake kwa Yehova naye daima hufuata kanuni za uadilifu. Anaweza kutunza siri. Pia, ni mkaribishaji wageni, yuko tayari kujitolea yeye mwenyewe na mali yake ili kuwanufaisha wengine.—Mdo. 20:33-35.

Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
Toka
Ingia
  • Kiswahili
  • Shiriki
  • Mapendezi
  • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
  • Masharti ya Utumiaji
  • Sera ya Faragha
  • Mpangilio wa Faragha
  • JW.ORG
  • Ingia
Shiriki