Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • Je! Wewe Wastahili Kutumikia?
    Mnara wa Mlinzi—1990 | Septemba 1
    • 16 Mwenye kiasi katika mazoea; mwenye kujidhibiti. (1 Timotheo 3:2; Tito 1:8, NW) Mzee apaswa kuwa mwenye tabia zenye uongozi mzuri, si mwenye kuwa mtumwa wa mazoea mabaya. Akabilipo majaribu, Mungu atamsa-idia adumishe usawaziko akisali kama mtunga zaburi: “Misononeko ya moyo wangu imezidika; O unitoe katika mikazo iliyo juu yangu.” (Zaburi 25:17, NW) Mwangalizi apaswa asali sikuzote kupata roho ya Mungu na aonyeshe tunda layo, kutia na kujidhibiti. (Luka 11:13; Wagalatia 5:22, 23) Kuwa mwangalifu juu ya fikira, usemi, na vitendo huwezesha mzee aepuke mambo ya kupita kiasi wakati aandaliapo kundi mwongozo wa kiroho.

  • Je! Wewe Wastahili Kutumikia?
    Mnara wa Mlinzi—1990 | Septemba 1
    • 19 Mkaribishaji wa wageni. (1 Timotheo 3:2; Tito 1:8, NW) Mzee ‘hufuata mwendo wa ukaribishaji wa wageni.’ (Warumi 12:13; Waebrania 13:2, NW) Neno la Kigiriki la “mkaribishaji wa wageni” humaanisha kwa uhalisi “mwenye kupenda wageni.” Hivyo, mzee aliye mkaribishaji wa wageni hukaribisha wapya kwenye mikutano ya Kikristo, akionyesha upendezi ule ule katika maskini kama afanyavyo katika walio na ufanisi wa vitu vya kimwili. Yeye ni mkaribishaji wa wageni kwa wale wanaosafiri kwa masilahi ya Ukristo na huwasindikiza “kama ipasavyo kwa Mungu.” (3 Yohana 5-8) Kwa kweli, mzee huonyesha ukaribishaji wa wageni hasa kwa waamini wenzake kulingana na mahitaji yao na kadiri hali zake ziruhusuvyo.—Yakobo 2:14-17.

  • Je! Wewe Wastahili Kutumikia?
    Mnara wa Mlinzi—1990 | Septemba 1
    • 23 Mpenda wema; mwadilifu. (Tito 1:8, NW) Ili astahili kuwa mzee, ni lazima mwanamume apende wema na awe mwadilifu. Mpenda wema hupenda kilicho chema machoni pa Yehova, hufanya matendo ya fadhili na yenye msaada, na huonyesha uthamini kwa wema wa wengine. (Luka 6:35; linganisha Matendo 9:36, 39; 1 Timotheo 5:9, 10.) Kuwa mwadilifu humaanisha kujipatanisha na sheria na viwango vya Mungu. Miongoni mwa mambo mengine, mwanamume wa jinsi hiyo hana upendeleo na hukumbuka mambo ya uadilifu, yaliyo safi kitabia, na yaliyo na nguvu za wema. (Luka 1:6; Wafilipi 4:8, 9; Yakobo 2:1-9) Kwa kuwa wema hutofautiana na uadilifu kwa kufanya mengi kuliko yale yatakwayo na haki, mpenda wema hufanyia wengine mengi kuliko yale yatakwayo kwake.—Mathayo 20:4, 13-15; Warumi 5:7.

      24 Mwaminifu-mshikamanifu. (Tito 1:8, NW) Mwanamume astahiliye kuwa mzee hudumisha ujitoaji usiovunjika kwa Mungu na hushikamana na sheria ya kimungu, hata kama ukamilifu-maadili wake watahiniwa jinsi gani. Yeye hufanya mambo ambayo Yehova hutarajia kwake, nayo ni kutia ndani kutumikia akiwa mpiga mbiu mwaminifu wa Ufalme.—Mathayo 24:14; Luka 1:74, 75; Matendo 5:29; 1 Wathesalonike 2:10.

Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
Toka
Ingia
  • Kiswahili
  • Shiriki
  • Mapendezi
  • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
  • Masharti ya Utumiaji
  • Sera ya Faragha
  • Mpangilio wa Faragha
  • JW.ORG
  • Ingia
Shiriki