Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • Kuhani Mkuu
    Ufahamu wa Kina wa Maandiko
    • Ukuhani Mkuu wa Yesu Kristo. Kitabu cha Waebrania kinataja kwamba tangu Yesu Kristo alipofufuliwa na kurudi mbinguni, aliwekwa kuwa “kuhani mkuu milele kama Melkizedeki.” (Ebr 6:20; 7:17, 21) Mwandikaji wa kitabu hicho anafafanua jinsi ukuhani wa Kristo ulivyo mkuu na bora kuliko ukuhani wa Haruni kwa kutaja kwamba Melkizedeki alikuwa mfalme na kuhani aliyechaguliwa na Mungu Aliye Juu Zaidi, bali si kupitia urithi. Kristo Yesu, hakutokana na kabila la Lawi, bali la Yuda katika ukoo wa Daudi, hivyo, hakurithi cheo hicho kutoka kwa Haruni, bali alikipata kwa kuteuliwa moja kwa moja na Mungu, kama Melkizedeki. (Ebr 5:10) Mbali na ahadi iliyo kwenye Zaburi 110:4: “Yehova ameapa naye hatabadili nia yake: ‘Wewe ni kuhani milele kwa mfano wa Melkizedeki!’” jambo linalomfanya kuwa Mfalme na Kuhani mbinguni, Kristo pia ana mamlaka ya Ufalme kwa sababu ni uzao wa Daudi. Na kwa sababu hiyo, anakuwa mrithi wa ufalme kupatana na ahadi ya agano la Daudi. (2Sa 7:11-16) Kwa hiyo, ana vyeo viwili, mfalme na kuhani, kama Melkizedeki.

      Ubora wa ukuhani wa Kristo unaonekana kupitia wazo la kwamba Lawi, ambaye alitokeza ukoo wa makuhani Wayahudi, alimpa Melkizedeki sehemu ya kumi, kwa maana bado Lawi alikuwa katika viuno vya Abrahamu alipompa sehemu ya kumi mfalme wa Salemu aliyekuwa pia kuhani. Isitoshe, hilo linamaanisha kwamba Lawi alibarikiwa pia na Melkizedeki, na ukweli ni kwamba mdogo hubarikiwa na mkubwa. (Ebr 7:4-10) Vilevile, mtume Paulo anataja kwamba Melkizedeki “hana baba wala mama, hana ukoo, na hana mwanzo wa siku wala mwisho wa uzima” akiwakilisha ukuhani wa milele wa Yesu Kristo, ambaye amefufuliwa na kupewa “uzima usioweza kuharibika.”​—Ebr 7:3, 15-17.

  • Kuhani Mkuu
    Ufahamu wa Kina wa Maandiko
    • Makuhani Wakristo wa Cheo cha Chini. Yesu Kristo ndiye kuhani pekee aliye “mfano wa Melkizedeki” (Ebr 7:17), lakini kama ilivyokuwa kwa Haruni kuhani mkuu wa Israeli, Yesu Kristo ana kikundi cha makuhani wa cheo cha chini aliopewa na Yehova, Baba yake. Makuhani hao wameahidiwa kuwa warithi pamoja naye mbinguni, ambako watashiriki pia kuwa wafalme katika Ufalme wake. (Ro 8:17) Wanajulikana kuwa “ukuhani wa kifalme.” (1Pe 2:9) Katika maono ya kitabu cha Ufunuo wanaimba wimbo mpya na kusema kwamba Kristo aliwanunua kwa damu yake na “[ku]wafanya kuwa ufalme na makuhani kwa Mungu wetu, [na kwamba] watatawala wakiwa wafalme juu ya dunia.” (Ufu 5:9, 10) Baadaye, maono hayo yanaonyesha kwamba idadi yao ni 144,000. Vilevile wanafafanuliwa kuwa “wamenunuliwa kutoka duniani,” wakiwa wafuasi wa Mwanakondoo, ambao “walinunuliwa kutoka kati ya wanadamu wakiwa matunda ya kwanza kwa Mungu na kwa Mwanakondoo.” (Ufu 14:1-4; linganisha Yak 1:18.) Katika sura hiyo ya kitabu cha Ufunuo (14), onyo linatolewa kuhusu alama ya mnyama wa mwituni, na hivyo kuonyesha kwamba “watakatifu [watahitaji] uvumilivu” ili kukataa alama hiyo. (Ufu 14:9-12) Wale 144,000 ambao wamenunuliwa ndio wanaovumilia kwa uaminifu, kisha wanakuwa hai na kutawala wakiwa wafalme pamoja na Kristo, nao “watakuwa makuhani wa Mungu na wa Kristo, nao watatawala wakiwa wafalme pamoja naye ile miaka 1,000.” (Ufu 20:4, 6) Utumishi wa Yesu akiwa kuhani mkuu unawasaidia kufikia cheo hicho chenye utukufu.

Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
Toka
Ingia
  • Kiswahili
  • Shiriki
  • Mapendezi
  • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
  • Masharti ya Utumiaji
  • Sera ya Faragha
  • Mpangilio wa Faragha
  • JW.ORG
  • Ingia
Shiriki