-
Wazee Ilindeni Amana YenuMnara wa Mlinzi—1989 | Septemba 15
-
-
12. Ni shauri gani lililotangazwa kwa chapa wakati mmoja katika jarida hili ambalo litasaidia mzee aepuke kutumia vibaya ulimi?
12 Linda amana yako ukiwa mzee, kwa kuepuka mitego pia. Mmojapo ni kutumia vibaya ulimi ukiwa mwalimu. Uhitaji wa hadhari katika jambo hili umekaziwa kwa muda mrefu na tengenezo la Yehova. Kwa kielelezo, katika toleo la Mei 15, 1897, jarida hili lilizungumzia Yakobo 3:1-13 na kusema hivi kuhusu wazee hasa: “Wakiwa na ulimi wenye ufasaha unaweza kuwa mfereji wa kuleta baraka kubwa, ukigeuza hesabu kubwa za watu wamwelekee Bwana, ukweli na njia ya uadilifu; au, kwa upande mwingine, ukiwa umechafuliwa kwa kutiwa makosa, ulimi unaweza kuleta madhara yasiyoweza kuelezeka—kuumiza imani, maadili, kazi zilizo njema. Hakika ni kweli kwamba, yeyote anayejizoeza kipawa cha kufundisha anajifunua wazi kwenye daraka zaidi machoni pa Mungu na wanadamu. . . .Yeyote ambaye angekuwa chemchemi ambayo kutoka kwayo Neno la kimungu lingetoka, akileta baraka na burudisho na imara, yapasa ahakikishe kwamba maji machungu, mafundisho bandia ambayo yangeweza kusababisha laana, au umizo—kutomheshimu Mungu na kupotosha Neno lake—hayapasi kupata mfereji wa kutokea ili yatamkwe. Katika kuchagua viongozi wa mikutano sifa ya ‘ulimi’ kama ilivyoonyeshwa hapa haipasi kusahauliwa. Walio na ulimi moto hawapasi kuchaguliwa, bali ni wale tu walio wasikivu, wenye kiasi zaidi, ‘wanaotia lijamu’ katika ndimi zao na kujitahidi kwa uangalifu ‘kunena kama waneni wenye kuwakilisha Mungu.’” Ni jambo la maana kama nini mzee atumie ulimi wake kwa njia halali!
-
-
Wazee Ilindeni Amana YenuMnara wa Mlinzi—1989 | Septemba 15
-
-
17, 18. Ni shauri gani lililotangazwa kwa chapa katika gazeti hili miaka 80 hivi iliyopita ambalo bado linatumika kwa wazee Wakristo?
17 Zaidi ya miaka 80 iliyopita, Mnara wa Mlinzi (Machi 1, 1909, kwa Kiingereza) ilinukuu shauri la Paulo linalotangulia kwa wazee wenzi na kueleza hivi: “Wazee walio kila mahali wanahitaji kutii kwa njia ya pekee; kwa sababu katika kila jaribu wale wanaopendelewa sana na walio mashuhuri sana wanashambuliwa na kutahiniwa vikali. Kwa sababu hiyo [Yakobo] anasihi hivi, ‘Wengi wenu msiwe walimu, akina ndugu, mkijua ya kwamba mtu atapokea mtihani mkali zaidi.’ Sisi, vilevile, tunawasihi Wazee wote ambao wana moyo wenye kutakata, usio na ubinafsi, kwamba wasiwe na jambo lolote isipokuwa upendo na kuwatakia mema aina yote ya binadamu, na kwamba wajazwe zaidi na zaidi na matunda na neema za Roho takatifu, wakilitii kundi pia. Kumbukeni kwamba, kundi ni la Bwana na kwamba nyinyi mna daraka kwa Bwana, na pia kwao. Kumbukeni kwamba, nyinyi mnapaswa kuangalia nafsi (masilahi) zao kama wale ambao lazima watoe hesabu kwa Mchungaji Mkubwa aliye Mkuu. Kumbukeni kwamba, jambo kuu ni Upendo, katika yote; na, huku mkiwa hamwachilii mafundisho, uangalieni kwa njia ya pekee ukuzi wa Roho wa Bwana miongoni mwa washiriki mbalimbali wa Mwili wake, ili kwamba waweze ‘kupata urithi wa watakatifu katika nuru,’ na, kulingana na penzi la Kimungu, wasiteseke kwa kujikwaa katika siku hii mbovu, bali, wakiwa wamekwisha kufanya yote, wasimame wakiwa kamili katika Kristo, Mwili wake, Washiriki wake, Watoa-Dhabihu-Waungani wake, Warithi-Waungani wake.”
-