Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • Mwongozo Wenye Hekima kwa Wenzi wa Ndoa
    Mnara wa Mlinzi—2005 | Machi 1
    • 15, 16. Mke Mkristo anaweza kumvuta mume asiyeamini kwa mwenendo wa aina gani?

      15 Ni mwenendo wa aina gani unaoweza kumvuta mume? Kwa kweli, ni mwenendo ambao kwa kawaida husitawishwa na wanawake Wakristo. Petro anasema: “Kujipamba kwenu kusiwe kule kusuka nywele kwa nje na kule kujivika mapambo ya dhahabu au kuvaa mavazi ya nje, bali kuwe yule mtu wa siri wa moyoni katika vazi lisiloharibika la roho ya utulivu na ya upole, ambayo ni ya thamani kubwa machoni pa Mungu. Kwa maana, pia, ndivyo walivyokuwa wakijipamba wale wanawake watakatifu hapo zamani, waliokuwa wakimtumaini Mungu, wakijitiisha kwa waume zao wenyewe, kama Sara alivyokuwa akimtii Abrahamu, akimwita ‘bwana.’ Nanyi mmekuwa watoto wake, mradi tu mnaendelea kutenda mema na kutokuwa na woga kwa sababu ya kitisho chochote.”—1 Petro 3:3-6.

  • Mwongozo Wenye Hekima kwa Wenzi wa Ndoa
    Mnara wa Mlinzi—2005 | Machi 1
    • 17. Sara ni kielelezo kizuri kwa wake Wakristo jinsi gani?

      17 Sara anatajwa kuwa kielelezo, naye ni mfano mzuri wa kuigwa na wake Wakristo iwe waume zao ni waamini au la. Bila shaka, Sara alimwona Abrahamu kuwa kichwa chake. Hata moyoni mwake, alimwita “bwana” wake. (Mwanzo 18:12) Hata hivyo, hilo halikumfanya kuwa duni. Ni wazi kwamba alikuwa mwanamke mwenye nguvu kiroho aliyekuwa na imani thabiti katika Yehova. Kwa kweli, yeye ni sehemu ya ‘wingu kubwa la mashahidi’ ambao kielelezo chao cha imani kinapaswa kutuchochea “tukimbie kwa uvumilivu shindano la mbio lililowekwa mbele yetu.” (Waebrania 11:11; 12:1) Kwa hiyo mke Mkristo hawi duni anapomwiga Sara.

Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
Toka
Ingia
  • Kiswahili
  • Shiriki
  • Mapendezi
  • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
  • Masharti ya Utumiaji
  • Sera ya Faragha
  • Mpangilio wa Faragha
  • JW.ORG
  • Ingia
Shiriki