-
Kapadokia—Mahali Ambapo Watu Waliishi Katika Nyumba Zilizochongwa na Upepo na MajiMnara wa Mlinzi—2004 | Julai 15
-
-
MTUME Petro alitaja Kapadokia. Kati ya watu aliowaandikia barua yake ya kwanza iliyoongozwa na roho ya Mungu ni “wakaaji wa muda waliotawanyika huku na huku katika . . . Kapadokia.” (1 Petro 1:1) Kapadokia ilikuwa nchi ya aina gani? Kwa nini wakaaji wake waliishi kwenye nyumba zilizochongwa katika mawe? Ukristo uliwafikiaje?
-
-
Kapadokia—Mahali Ambapo Watu Waliishi Katika Nyumba Zilizochongwa na Upepo na MajiMnara wa Mlinzi—2004 | Julai 15
-
-
Kufikia karne ya pili K.W.K., kulikuwa na jamii za Wayahudi huko Kapadokia. Na Wayahudi kutoka eneo hilo walikuweko Yerusalemu mnamo mwaka wa 33 W.K. Walikuwa huko ili kusherehekea Sherehe ya Pentekoste. Hivyo, mtume Petro aliwahubiria Wayahudi wa Kapadokia baada ya roho takatifu kumwagwa. (Matendo 2:1-9) Yaelekea baadhi yao walikubali ujumbe wake na wakawaeleza wenzao imani yao mpya waliporudi makwao. Hivyo, katika barua yake ya kwanza Petro alikuwa akizungumza na Wakristo wa Kapadokia.
-