-
Ukombozi Wakaribia kwa Ajili ya Watu wa Ujitoaji Kimungu!Mnara wa Mlinzi—1990 | Aprili 15
-
-
2, 3. (a) Ni kwa nini sisi leo tunaona yale yanayosemwa kwenye 2 Petro 2:9 kuwa yenye kutupa uhakika? (b) Biblia inaelekeza kwenye matendo gani hususa ya ukombozi kuwa msingi wa kitia-moyo?
2 Yanayotukia katika siku yetu hutuku-mbusha nyakati nyingine zenye umaana mkubwa katika historia ya kibinadamu. Mtume Petro huvuta uangalifu kwenye matendo ya ukombozi ambayo Mungu alifanya katika pindi hizo, kisha anaelekeza kwenye neno mkataa hili lenye kutoa uhakikisho: “Yehova ajua jinsi ya kukomboa watu wa ujitoaji kimungu katika jaribu.” (2 Pet. 2:9, NW) Angalia maneno yanayozunguka taarifa hiyo kwenye 2 Petro 2:4-10, NW:
3 “Kwa hakika ikiwa Mungu hakukosa kuadhibu malaika waliofanya dhambi, bali, kwa kuwatupa katika Tartaro, aliwapeleka kwenye mashimo yenye giza zito mno wawekwe akiba kwa ajili ya hukumu; na yeye hakukosa kuadhibu ulimwengu wa kale, bali alimlinda Noa, mhubiri wa uadilifu, salama pamoja na wengine saba wakati alipoleta gharika juu ya ulimwengu wa watu wasiohofu Mungu; na kwa kuyafanya majiji ya Sodoma na Gomora kuwa majivu aliwalaani, akiweka kiolezo kwa ajili ya watu wasiohofu Mungu cha mambo yatakayokuja; naye alimwokoa Loti mwadilifu, aliyesumbuliwa sana na anasa ya mwenendo mlegevu wa watu wakaidi-sheria—maana mtu huyo mwadilifu kwa yale aliyoona na kusikia alipokuwa akikaa miongoni mwao siku kwa siku alikuwa akitesa nafsi yake yenye uadilifu kwa sababu ya matendo yao yasiyo ya kisheria—Yehova ajua jinsi ya kukomboa watu wa ujitoaji kimungu katika jaribu, lakini kuwaweka akiba watu wasio waadilifu kwa ajili ya siku ya hukumu wakatiliwe mbali, hata hivyo, hasa wale wanaofuata mnofu pamoja na tamaa ya kuuchafua na wanaodharau ubwana.” Kama yanavyoonyesha maandiko hayo, yaliyotukia katika siku za Noa na katika wakati wa Loti yanajaa maana kwetu.
-
-
Ukombozi Wakaribia kwa Ajili ya Watu wa Ujitoaji Kimungu!Mnara wa Mlinzi—1990 | Aprili 15
-
-
4. Katika siku ya Noa, ni kwa nini Mungu aliona dunia kuwa imeharibiwa? (Zaburi 11:5)
4 Habari ya kihistoria katika Mwanzo sura ya 6 hutupasha habari kwamba katika siku ya Noa dunia ilikuja kuharibika machoni pa Mungu wa kweli. Kwa nini? Kwa sababu ya jeuri. Hilo halikuwa jambo la visa vya hapa na pale vya jeuri ya uhalifu. Mwanzo 6:11, NW huripoti kwamba “dunia ikajaa jeuri.”
5. (a) Ni mtazamo gani kwa upande wa binadamu ulichangia jeuri ya siku za Noa? (b) Enoki alikuwa ameonya nini kwa habari ya hali ya kutohofu Mungu?
5 Ni nini kilichoisababisha? Andiko ambalo limenakiliwa kutoka 2 Petro hutaja watu wasiohofu Mungu. Ndiyo, roho ya kutohofu Mungu ilijaa katika mambo ya binadamu. Hiyo ilihusu si kutojali tu sheria ya kimungu kwa ujumla bali mtazamo wa ukaidi kuelekea Mungu mwenyewe.a Na watu wanapokuwa wakaidi kuelekea Mungu, inaweza kutarajiwaje kwamba watashughulika na wanadamu wenzao kwa fadhili? Tayari kabla Noa kuzaliwa, kutohofu Mungu huku kulitokeza sana hivi kwamba Yehova alimfanya Enoki atoe unabii kuhusu matokeo. (Yuda 14, 15, NW) Kukaidi Mungu kwao hakika kungeleta utekelezo wa hukumu ya kimungu.
-
-
Ukombozi Wakaribia kwa Ajili ya Watu wa Ujitoaji Kimungu!Mnara wa Mlinzi—1990 | Aprili 15
-
-
a “Anomia ni kutojali, au kukaidi, sheria za Mungu; asebia [namna ya nomino ya neno lililotafsiriwa ‘watu wasiohofu Mungu’] ni mtazamo uo huo kuelekea Mungu mwenyewe.”—Vines Expository Dictionary of Old and New Testament Words, Buku 4, ukurasa 170.
-