Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • Inamaanisha Nini Kutounga Mkono Upande Wowote
    Furahia Maisha Milele!—Masomo ya Kujifunza Biblia
    • 2. Tunawezaje kuonyesha kwamba hatuungi mkono upande wowote?

      Kama Yesu, sisi pia hatujihusishi na siasa. Watu walipoona muujiza mmoja wa Yesu, walitaka kumfanya awe Mfalme wao duniani, lakini alikataa. (Yohana 6:15) Kwa nini alikataa? Kwa sababu baadaye alisema hivi: “Ufalme wangu si sehemu ya ulimwengu huu.” (Yohana 18:36) Tukiwa wanafunzi wa Yesu, tunaonyesha kwa njia mbalimbali kwamba hatuungi mkono upande wowote. Kwa mfano, hatushiriki katika vita. (Soma Mika 4:3.) Tunaheshimu nembo za taifa kama vile bendera, lakini hatuziabudu. (1 Yohana 5:21) Na hatuungi mkono wala kupinga mgombeaji au chama chochote cha kisiasa. Kwa kufanya hivyo, tunaonyesha kwamba sisi ni washikamanifu kabisa kwa serikali ya Mungu, yaani, Ufalme wake.

  • Inamaanisha Nini Kutounga Mkono Upande Wowote
    Furahia Maisha Milele!—Masomo ya Kujifunza Biblia
    • 4. Onyesha kwamba huungi mkono upande wowote kupitia mawazo na matendo yako

      Soma 1 Yohana 5:21. Kisha, onyesha VIDEO na mzungumzie maswali yanayofuata.

      VIDEO: Wakristo wa Kweli Wanahitaji Ujasiri​—Ili Wasiunge Mkono Upande Wowote (2:50)

      • Katika video hiyo, kwa nini Ayenge alikataa kujiunga na chama cha kisiasa au kushiriki katika sherehe za kitaifa, kama vile kupiga saluti mbele ya bendera?

      • Je, unafikiri alifanya uamuzi wa hekima?

      Msimamo wetu wa kutounga mkono upande wowote unaweza kujaribiwa katika hali gani nyingine? Onyesha VIDEO, kisha mzungumzie maswali yanayofuata.

      VIDEO: Masomo Kutoka kwa Mnara wa Mlinzi​—Usiunge Mkono Upande Wowote Katika Ulimwengu Huu Uliogawanyika (5:16)

      • Tunawezaje kuonyesha kwamba hatuungi mkono upande wowote kunapokuwa na mashindano ya michezo kati ya mataifa mbalimbali?

      • Tunawezaje kuendelea kutounga mkono upande wowote, iwe maamuzi ya wanasiasa yatatunufaisha au kutuletea madhara?

      • Msimamo wetu wa kutounga mkono upande wowote unawezaje kuathiriwa na mambo tunayosikia katika vyombo vya habari au watu tunaoshirikiana nao?

      Picha: 1. Kikundi cha watu wenye hasira walio na mabango wakiandamana. 2. Mwanamume akishangilia akiwa ameshika bendera wakati wa mashindano ya michezo. 3. Mwanafunzi anaimba wimbo wa taifa. 4. Mwanajeshi akiwa amebeba bunduki. 5. Wagombeaji wawili wa kisiasa wakifanya mjadala. 6. Mwanamke anaweka kura katika sanduku wakati wa kupiga kura.

      Ni katika hali gani ambazo Mkristo anapaswa kudumisha msimamo wa kutounga mkono upande wowote kupitia mawazo na matendo yake?

Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
Toka
Ingia
  • Kiswahili
  • Shiriki
  • Mapendezi
  • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
  • Masharti ya Utumiaji
  • Sera ya Faragha
  • Mpangilio wa Faragha
  • JW.ORG
  • Ingia
Shiriki