-
Ya Mwisho ya Zile Serikali Kubwa za UlimwenguMnara wa Mlinzi—1988 | Mei 15
-
-
Wakati kitabu cha Biblia cha Ufunuo kilipoandikwa, takriban miaka 1,900 iliyopita, kilisema kwamba “wafalme” watano, au serikali kubwa za ulimwengu, zilikuwa tayari zimekuja na kwisha. Hizo zilikuwa Misri, Ashuru, Babuloni, Umedi-Uajemi, na Ugiriki. Ile ya sita, Roma, ‘ilikuwako’ bado, lakini ya saba ilikuwa haijawasili. (Ufunuo 17:10, NW) Hiyo serikali kubwa ya saba ya ulimwengu ilikuwa nini? Ilikujaje kuwako? Na ni nini itakayoifuata? Majibu kwa maswali haya ya maana ndiyo habari ya makala hii.
-
-
Ya Mwisho ya Zile Serikali Kubwa za UlimwenguMnara wa Mlinzi—1988 | Mei 15
-
-
Kisiwa kimoja katika pembe ya kaskazini-magharibi ya Milki ya Roma kilikuwa kimebaki kando bila kuhusishwa sana katika mambo ya ulimwengu. Ni kama vile mwanahistoria mmoja alivyoeleza: “Katika karne ya kumi na sita Uingereza ilikuwa imekuwa serikali ya kikawaida tu. Utajiri wayo ulikuwa hafifu ukilinganishwa na ule wa Uholanzi. Idadi ya watu wayo ilikuwa kidogo sana kuliko ile ya Ufaransa. Kani zayo za kijeshi (kutia na jeshi la baharini) zilikuwa duni kwa zile za Hispania.” Hata hivyo, Uingereza ilisitawisha kikosi cha baharini chenye umashuhuri fulani, na maharamia wayo wa baharini, na meli za watu binafsi, wakaanza kuvamia makoloni ya Hispania na meli zao zilizojazwa hazina.
Zile Pembe Tatu
Katika 1588 Phillip 2 wa Hispania aliondokesha kile kikosi cha meli za Armada cha Hispania dhidi ya watesi wake Waingereza. Kikosi hiki cha meli 130 chenye kuchukua wanaume zaidi ya 24,000 kilisafiri polepole kikielekea juu katika ule Mfereji wa Uingereza, kumbe kikakabiliwa na pepo na dhoruba kali-kali za Atlantiki. Katika Modern Europe to 1870, mwanahistoria Carlton Hayes anaandika kwamba tukio hili “lilikuwa ndiyo hatua ya kukata maneno ambapo uhodari wa meli za kijeshi uliacha kuwa wa Hispania ukawa wa Uingereza.”
Katika karne ya 17, Waholanzi walisitawisha kikosi cha meli za ubiashara chenye ukubwa unaovizidi kwa mbali vikosi vinginevyo vyote ulimwenguni. Meli zao ndizo zilizozitawala bahari, nazo zilisaidia kufikisha faida zao kwenye serikali za kote kote. Lakini Uingereza ikawa ndiyo yenye nguvu zaidi katika jambo hili pia, kwa sababu ya kuongezeka kwa makoloni yake ya ng’ambo.
Ndipo, katika karne ya 18, Waingereza na Wafaransa walipigana wakiwa sehemu za mbali mbali sana kama Amerika ya Kaskazini na India, na hiyo ikaongoza kwenye ule Mkataba wa Paris katika 1763. Kuhusu mkataba huo, William B. Willcox aliandika katika kitabu chake Star of Empire—A Study of Britain as a World Power kwamba ingawa mkataba huo ulionekana kama kuacha msimamo wa kwanza, “kwa kweli ulitambua msimamo mpya wa Uingereza kuwa ndiyo serikali kubwa zaidi ya Ulaya katika ulimwengu uliokuwa ng’ambo ya Ulaya.”
Wanahistoria wengine wanaafikiana na jambo hilo, wakisema: “Kutokana na karne mbili za kufanya vita pamoja na Wahispania, Waholanzi, na Wafaransa, Uingereza Kuu iliibuka katika 1763 ikiwa ndiyo serikali ya mbele zaidi kibiashara na kikoloni katika ulimwengu.” (Modern Europe to 1870) “Katika 1763 Milki ya Uingereza ilitagaa kwa kukanyaga ulimwengu ikiwa kwa namna fulani kama Roma iliyohuishwa na kupanuliwa.” “Iliibuka katika vile vita vya katikati ya karne ile ikawa ndiyo milki iliyo kubwa na yenye imara kupita zote—tena ikiwa ndiyo serikali kubwa yenye kuchukiwa kabisa kuliko zote.” (Navy and Empire, kilichotungwa na James L. Stokesbury) Ndiyo, ‘pembe ndogo’ hii ilikuwa imekua ikawa ndiyo serikali kubwa ya saba ya ulimwengu katika historia ya Biblia.
-
-
Ya Mwisho ya Zile Serikali Kubwa za UlimwenguMnara wa Mlinzi—1988 | Mei 15
-
-
Yaliyo mengi ya makoloni ya Uingereza yamepata uhuru na kujiunga na Jumuiya ya Madola. Ingawa huenda milki yenyewe ikawa imeisha, ile Serikali Kubwa ya Ulimwengu ya Waingereza-Waamerika ingali ipo. Lakini itakuwako kwa “kitambo kidogo” tu, inapolinganishwa na zile karne nyingi ambazo serikali kubwa ya Kiroma iliyoitangulia ilidhibiti utawala.—Ufunuo 17:10, NW.
-