-
Siku ya Hukumu ya Mungu—Matokeo Yayo Yenye Shangwe!Ufunuo—Upeo Wao Mtukufu U Karibu!
-
-
7, 8. (a) Ni hati-kunjo gani inayofunguliwa, na ni jambo gani linalotukia baada ya hapo? (b) Ni kwa akina nani hakutakuwa na ufufuo?
7 Yohana anaongeza: “Lakini hati-kunjo nyingine ikafunguliwa; ndiyo hati-kunjo ya uhai. Na wafu walihukumiwa kutoka kwa vile vitu vilivyoandikwa katika hati-kunjo kulingana na matendo yao. Na bahari ikatoa wafu wale walio ndani yayo na kifo na Hadesi vikatoa wafu wale walio ndani yavyo na wao walihukumiwa mmoja mmoja kulingana na matendo yao.” (Ufunuo 20:12b, 13, NW) Tamasha yenye kusisimua kweli kweli! ‘Bahari, kifo, na Hadesi’ kila mojapo inatimiza sehemu, lakini angalia kwamba semi hizi si za pekee baina yazo zenyewe.a Wakati Yona alipokuwa tumboni mwa samaki mmoja na kwa hiyo akawa katikati ya bahari, yeye alisema juu yake mwenyewe kuwa alikuwa katika Sheoli, au Hadesi. (Yona 2:2) Ikiwa mtu anashikwa na kifo cha Adamu, basi yaelekea yeye pia yumo katika Hadesi. Maneno haya ya kiunabii yanatoa uhakikisho imara kwamba hakuna hata mmoja atakayekosa kuonwa.
-
-
Siku ya Hukumu ya Mungu—Matokeo Yayo Yenye Shangwe!Ufunuo—Upeo Wao Mtukufu U Karibu!
-
-
a Wale wanaofufuliwa kutoka katika bahari hawangetia ndani wakazi wafisadi wa dunia walioangamia katika Gharika ya siku ya Noa; uharibifu huo ulikuwa wa kukata maneno, kama utakavyokuwa utekelezo wa hukumu ya Yehova katika dhiki kubwa.—Mathayo 25:41, 46; 2 Petro 3:5-7.
-