Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • Ziwa la Moto Ni Nini? Je, Ni Sawa na Moto wa Mateso au Gehena?
    Maswali ya Biblia Yajibiwa
      • Kifo. (Ufunuo 20:14) Kifo si kitu halisi lakini ni hali ya kutotenda, kutokuwepo kwa uhai. (Mhubiri 9:​10) Kifo hakiwezi kuteketezwa.

  • Ziwa la Moto Ni Nini? Je, Ni Sawa na Moto wa Mateso au Gehena?
    Maswali ya Biblia Yajibiwa
    • Mfano wa uharibifu wa milele

      Biblia inasema kwamba ziwa la moto “linamaanisha kifo cha pili.” (Ufunuo 20:14; 21:8) Kifo cha kwanza kinachotajwa katika Biblia kilisababishwa na dhambi ya Adamu. Kifo hicho kinaweza kubadilishwa kupitia ufufuo na mwishowe kitamalizwa na Mungu.​—1 Wakorintho 15:21, 22, 26.

      Hakuna mtu anayeweza kutoka katika ziwa la moto la mfano

      Ziwa la moto linawakilisha kifo cha aina tofauti, au cha pili. Ingawa kifo hicho kinawakilisha hali ya kutotenda kabisa, ni tofauti na kifo cha kwanza kwa sababu Biblia haisemi lolote kuhusu ufufuo kutokana na kifo cha pili. Kwa mfano, Biblia inasema kwamba Yesu ana “funguo za mauti na za kuzimu [au, moto wa mateso],” kuonyesha kwamba ana mamlaka ya kuwafungua watu kutokana na kifo kinacholetwa kutokana na dhambi ya Adamu. (Ufunuo 1:​18; 20:13, Union Version) Hata hivyo, Yesu hana funguo za ziwa la moto wala hakuna mtu aliye na funguo hizo. Ziwa hilo la mfano linawakilisha adhabu ya milele inayoletwa kupitia uharibifu wa milele.​—2 Wathesalonike 1:9.

Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
Toka
Ingia
  • Kiswahili
  • Shiriki
  • Mapendezi
  • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
  • Masharti ya Utumiaji
  • Sera ya Faragha
  • Mpangilio wa Faragha
  • JW.ORG
  • Ingia
Shiriki