-
Je! Jina Lako Limo Katika Kitabu cha Uhai?Ufunuo—Upeo Wao Mtukufu U Karibu!
-
-
10. Ni jambo gani lenye kutia-moyo aliloona Yesu katika kundi katika Sardisi, na hilo limepasa lituathirije sisi?
10 Maneno ya Yesu yanayofuata kwa kundi la Sardisi yanatia moyo zaidi sana. Yeye anasema: “Hata hivyo, wewe una majina machache katika Sardisi ambayo hayakuchafua mavazi yao ya nje, nao watatembea pamoja na mimi katika meupe, kwa sababu wao wanastahiki. Yeye ambaye hushinda atapambwa hivyo mavazi ya nje meupe; na mimi kwa njia yoyote sitafuta jina lake kutoka kitabu cha uhai, bali mimi nitakiri jina lake mbele za Baba yangu na mbele ya malaika zake.” (Ufunuo 3:4, 5, NW) Je! maneno haya hayatuamshi na kuimarisha azimio letu la kuwa waaminifu? Kwa sababu ya uzembe upande wa baraza la wazee, kundi kwa ujumla huenda likaingia ndani ya usingizi wa kiroho. Hata hivyo, baadhi ya watu mmoja mmoja humo huenda wakajitahidi kishujaa kutunza utambulisho wao wa Kikristo ukiwa safi na bila kutiwa madoa na hivyo waendelee kuwa na jina zuri pamoja na Yehova.—Mithali 22:1.
-
-
Je! Jina Lako Limo Katika Kitabu cha Uhai?Ufunuo—Upeo Wao Mtukufu U Karibu!
-
-
13. Ni baraka gani zilizo akibani kwa Wakristo wapakwa-mafuta ambao ‘hawachafui mavazi yao ya nje’?
13 Wale katika Sardisi ambao ni waaminifu mpaka mwisho na hawachafui utambulisho wao wa Kikristo wanafikia utimizo wa tumaini zuri ajabu. Baada ya kusimamishwa kwa Ufalme wa Kimesiya katika 1914, wanafufuliwa kwenye uhai wa kiroho na wakiwa washindi hupambwa mavazi meupe ya nje yakiwa ufananisho wa uadilifu wao usio na kasoro, wala waa. Wakiwa wamekwisha tembea katika ile njia yenye kusonga iongozayo kwenye uhai, watafurahia thawabu ya milele.—Mathayo 7:14; Ona pia Ufunuo 6:9-11.
Milele Katika Kitabu cha Uhai!
14. Kitabu cha uhai ni nini, na ni majina ya akina nani yaliyorekodiwa humo?
14 “Kitabu cha uhai,” ni nini na ni majina ya akina nani yatakayotunzwa humo? Kitabu, au hati-kunjo, cha uhai hurejezea rekodi ya watumishi wa Yehova wanaokuja katika mstari wa kupokea tuzo la uhai wa milele. (Malaki 3:16) Humu katika Ufunuo rejezo mahususi limefanywa kwenye majina ya Wakristo wapakwa-mafuta. Lakini majina ya wale walio katika mstari wa uhai wa milele duniani yamerekodiwa pia humo. Zaidi ya hilo, majina yanaweza ‘kufutwa’ katika kitabu hicho. (Kutoka 32:32, 33) Hata hivyo, wale wa jamii ya Yohana ambao majina yao yanabaki katika kile kitabu cha uhai mpaka kifo chao wanapokea uhai usioweza kufa katika mbingu. (Ufunuo 2:10) Haya ndiyo majina ambayo Yesu anakiri hasa mbele za Baba yake na mbele ya malaika Zake. Lo! ni kubwa mno jinsi gani thawabu hiyo!
15. Washiriki wa ule umati mkubwa wataandikishaje majina yao bila kufutika katika kitabu cha uhai?
15 Ule umati mkubwa, ambao majina yao yameandikwa pia katika kitabu cha uhai, watatoka katika dhiki kubwa wakiwa hai. Kwa kuzoea imani muda wote wa Utawala wa Mileani wa Yesu na wakati wa mtihani wenye kukata maneno unaofuata, hawa watathawabishwa na uhai wa milele katika Paradiso duniani. (Danieli 12:1; Ufunuo 7:9, 14; 20:15; 21:4) Ndipo majina yao yatakapobaki yameandikwa bila kufutika katika kitabu cha uhai. Kwa kujua kinachotolewa hapa kwa njia ya roho takatifu, je! wewe huitikii kwa idili waadhi hii ya Yesu yenye kurudiwarudiwa: “Acheni yeye ambaye ana sikio asikie ambacho roho husema kwa makundi”?—Ufunuo 3:6, NW.
-